SEHEMU YA PILI
Basi katika kuendelea kutafakari kwangu, nalimuona kijana mmoja mtanashati mwerevu wa moyo aliekuwa akipendwa na kila mtu. Katika kuendelea kumtazama mwenendo wake alikuwa kijana mwenye tabia nzuri na mwaminifu sana. Kwa uaminifu wake mkubwa aliokuwa nao uliwafanya maboss zake wamwamini sana hadi kufikia kitendo cha kukabidhiwa idara nzima iwe chini yake. Mambo yalienda vizuri kwa kijana huyu uaminifu na ubora aliouonyesha ulimfanya atengeneze marafiki wengi huku maadui wakiongezeka pia.
Wakati namtazama kijana huyu niliona kundi kubwa la wafanyakazi wenzake wakimjadili kwa hasira na kuonyesha kwamba alikuwa kikwazo kikubwa cha wenzake kufanikiwa na kushindwa kupiga madili kwa uhuru wakimaaanisha kuvuna pesa na mali kwa njia ya wizi na udanganyifu.
Wakati naendelea kumtazama sauti ya mzee ilisikika “Mwanangu ukiamua kusimamia ukweli haimaanishi hautakuwa na maadui kwani shetani hajaenda likizo. Ukiwa rafiki wa MUNGU unakuwa adui wa shetani vice versa is true” alimalizia na maneno hayo ya kiingereza akimaanisha kinyume chake nisawa.
Wakati naendelea kutafakari kauli hiii na mwenendo mzima wa kijana huyu, macho yangu yalirudi na kumuona namna alivyoanza kuhangaika kuwaelesha watu na kutafuta namna ya kuwapendeza. Ghafla nilimuona akianguka kwenye mtego ambao wenzake waliusuka vyema, kwa kutaka kukwepa lawama aliamua kushirikiana nao na kupiga dili la pesa ndefu kidogo, huku moyo ukimuenda mbio akijua analolifanya sio sawa ila aliamua kufanya ili kuwapendeza wenzake. Dili hili lilijulikana na kijana huyu alipoteza uaminifu wake kwa maboss zake na wenzake ambao pia walimgeuka na kuanza kumkejeli. Boss wake alisikikitika sana hakuwa na la kufanya ilibidi afukuze kazi kijana huyu.
Nikiendelea kumtazama kijana alikuwa akiondoka huku mikono kaweka kichwani, mzee akaniambia “Moja ya mtego mkubwa ambao vijana huangukia nikutaka kueleweka na kila mtu, na kupendwa na kila mmoja, Tambua huwezi pendwa na kueleweka na kila mtu. Ukiamua kusimamia ukweli, lazima uache ubinafsi wa kutaka kupendwa na kueleweka na kila mmoja, hata marafiki zako wa karibu wanaweza wasikuelewe wote. Tambua jambo moja umeagizwa na kupewa jukumu la kupenda na sio kupendwa. Hivyo usiangahike na kupendwa hangaika na kupenda ndilo jukumu na wajibu wako.” “Kusimamia kweli ni moja ya kanuni ya upendo”
Aliniangalia kwa jicho la kipelelezi na kuendelea, mwanangu wako walioanza kunywa pombe ili kuwapendeza marafiki zao, wakaishi kuwa walevi na kuharibu maisha yao, maana kile apandacho mtu ndicho atakachovuna. Wako walikubali kulala na wachumba zao ilikuwapendeza huku wakijua wanachofanya sio sawa, wakaishia kuua na kuharibu ndoto zao kubwa. Wako walioishia kukubali kufanya mambo mengi ya aibu na mwisho wao ukaishia kuwa fumbo la Imani.
Mzee aliinua mkono wake aknishika bega akaniambia “Hakikisha kila maamuzi na majibu unayoyatoa kwenye changamoto unazopitia hayaui ndoto yako, wala kutengengeza changamoto nyingine baadae.”
Sulemani aliwahi kusema kwa wingi wa washauri nchi uokoka Bali lazima uwe na uhakika hayo mashauri lazima yawe mema, tofauti na hapo ni uangamivu wa taifa. Kama mti mwema usivyoweza kuzaa matunda mabaya au mwembe kuzaa mapapai ndivyo ilivyo mashauri mema hutoka kwa watu wema, jifanyie marafiki kwa watu wenye hekima nawe utakuwa na hekima Ila rafiki wa wapumbavu ataumia.
Wakati huu nilikaa kimya nikiyatafakari maneno haya, mzee aliongezea nikisema unajukumu la kupenda lazima uelewe maana ya upendo, ukitaka kuelew vyema kuhusu upendo rudi kwa alieagiza ambae ni MUNGU mwenyewe. Alivyomaliza kusema haya akakaa kimya kidogo.
Basi kumbukumbu na tafakari zangu zikarejea na kuona maboss wa kijana wakihitisha kikao cha dharura mmoja akasimama akasema tulikuwa tukimuandaa huyu kijana kwaajili ya kukaimu na baadae kuchukua nafasi yangu, lakini yote tuliyoyatumainia kwake yamepotea na kuharibika kwa kashfa kubwa aliejitengenezea kwa kuamua kushirikiana na watu wasio faa katika kuhiujumu taasisi yetu. Hivyo basi tuchague kijana mwingine atakaeshika nafasi hii.
Hapa sauti ya mzee ilisikika tena, ikisema angalia sana usipoteze thawabu yako ulieitengeneza kwa machozi na kwa mda mwingi kwa kushindwa kujisimamia tu. Heri mwisho mzuri kuliko mwanzo.
Mwanangu wengi wameharibu hatima zao kwa mikono yao wenyewe huku wakiishia kumlalamikia MUNGU bila kujua wao ndio walioharibu mchakato.
Mwanangu lazima ujue kuwa kunamchakato unaonekana na ule usioonekana, kutokuona matokeo kwa haraka haimainishi kuwa hakuna kinachoendelea, Bali humaanisha wakati wa kutokeza haujafika, hivyo ni jukumu lako kuendelea kuumwagilia na kuutunza mche wako hadi wake na majira yake ya kuzaa yatakapotimia. Basi usifukue hiyo mbegu, usiukate huo mti, usitie sumu wala kuacha kuutunza, bali juhudi na bidii za kuutunza zinapaswa zizidi Zaidi ili kuhakikisha unazaaa vyema na matunda yenye afya msimu wake ukifika.
Mwanangu usifukue hiyo mbegu ya uaminifu, hiyo mbegu ya uzalendo, hiyo mbegu ya Neno na Maombi, wala usikate huo mti wa huduma ulioanza kuchipuka, huo mti wa biashara au huo mti wako wa ndoa na familia, bali pambana na kuzuia pamoja na kutibu inapokumbwa na magonjwa bila kusahahu bidii katika kuutunza vyema. Utavuna usipozimia moyo.
Pia ninapenda ufahamu kuwa Kamwe Giza na nuru haviwezi kuchangamana, kwenye giza hakuna nuru na kwenye Nuru hakuna Giza, hivyo ukiamua kuwa nuru hakikisha hauyumbishwi na chochote ili upokee ujira wako kwa wakati wake sawasawa na kiwango cha uangavu wa nuru yako.
Wewe ni dhahabu haipingiki ila ukikataa na kuharibu mchakato unaweza ishia kuishi kama kokoto hadi pale utakapojitambua na kutubu na kurudi kwenye mstari.
Ila lazima ujue kubomoa ni jambo rahisi ila kujenga ni gharama na inachukua muda. Hivyo nikusihi hiyo dhahabu kubwa uliyonayo unapaswa kujua namna ya kuilinda katikati ya mchakato na wanyang’anyi njiani kuelekea kwenye ukuu wako.
Mwanangu hiyo bidii na juhudi ulizoanza kuhusu biashara, huduma, maombi, neno na kujitoa kwako kwenye mambo mema hupaswi kuacha kwani kubomoa ni rahisi ila kujenga nigharama hasa kukarabati nyufa zilizoachia.
Hakikisha huachi, huchoki wala hurudi nyuma, Bali uwe tayari kupambana na kila ugonjwa pamoja na maradhi yatakayokuja kuipiga hiyo juhudi ya mambo mema uyafanyayo.
Mwanangu nikukumbushe kitu, Adui akipiga juhudi zako kuhusu uchumi, amepiga uchumi wako, akipiga juhudi za zako kuhusu MUNGU amepiga kila kitu na kuharibu maendeleo yako. Ilikupiga na kuharibu hayo yote anaweza kuanza kwa kupiga maarifa uliyonayo yaliyomema na yanayokujenga. Si kila chakula unapaswa kula kuna vyakula vingine ukila umeua na kuharibu ndoto yako kwa mikono yako mwenyewe. Kuwa makini kwenye yale unayolisha ubongo wako.
Tambua hili kukosa kwa uaminifu kwa mtu mmoja kazini au nyumbani ni mlango wa kuleta majuto na madhara makubwa kwa familia, Taasisi na nchi kwa ujumla wake.
Sina mda wa kukueleza vizuri kuhusu madhara ya uaminifu, nakuahidi kukuandikia soon, Ila lazima utambue ukosefu wa uaminifu ni mshale uliorushwa gizani kuja kujeruhi na kuharibu maisha ya watu ikiwemo uchumi wao, ndoa, na mahusiano ya watu.
Mwanangu kwepa mshale huu kwa kuamua kuwa mwaminifu uokoe ndoto na maono yako. Usikubali mshale huu ukuue. Mwanangu usikubali kufa kibudu, inuka kimbia…
Mwanangu nimalizie kwa kukuambia ukweli huu kuwa uaminifu siku zote ni zao LA IMANI. Kiwango cha IMANI uliyonayo kwa MUNGU ndio itakayoamua kiwango Chako cha uaminifu kwenye eneo lolote. Kuwa na IMANI na Mungu ni kuamini yote aliyoyasema kuhusu Wewe mazuri na mabaya yatokanayo na utakayotenda na utakayoacha. Kwenda Kinyume ni udhihirisho tosha kuwa huaminia alichokisema. Ili kujenga uaminifu wako unapaswa kujenga IMANI yako kwa MUNGU wako. "JENGA IMANI KUJENGA UAMINIFU"
Ng’ombe akifa kabla ya kuchinjiwa tunamwita nyamafu hana faida tena hafai kuliwa, lakini akiwa amechinjwa tunaita nyama. Hii tunaifurahia na kuitumia kama kitoweo. Ng,ombe anaweza kufa kwa ugonjwa.
Usiruhusu ugonjwa huu na mshale huu wa mauti ujilikanao kama ukosefu wa uaminifu uue ndoto zako, uuaribu dhahabu kubwa ambayo MUNGU aliweka ndani yako Bali hakikisha unapambana kuona ndoto zako zikitimia.
Ukosefu wa uaminifu sio sifa, kutoka nje ya ndoa sio sifa huo ni mtego unaoua ndoto na maono ya familia nyingi. Shtuka ee kijana.
Hivyo usife kibudu hakikisha unapambana kukamilisha ndoto zako ili baada ya kufa uendelee kuishi ndani ya mioyo ya watu.
Iwe Amani na utele kwako.
NUKUU: Mathayo 25:23-28.
Uaminifu ulionao kwa MUNGU ndio utakaoamua umbali utakaoenda kwenye maisha yako. "Kumbuka njia ya muongo ni fupi, ndivyo ilivyo njia ya asiyekuwa mwaminifu."
Mithali 28:20 (KJV) Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; Lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa.
Ukikosa uaminifu, uongo ni fungi lako. Ukweli ni zao LA uaminifu, na uaminifu ni zao LA IMANI. MTU mwaminifu ni MTU aliejaa IMANI kwa MUNGU. Anaamini kile MUNGU alichosema zaidi ya mazingira yanavyoonyesha.
Mithali 14:5 (KJV) Shahidi mwaminifu hatasema uongo; Bali shahidi wa uongo, pumzi zake ni uongo.
MTU mwaminifu si yule ambaye hajakamatwa kwenye wizi au tendo lingine linaloashiria ukosefu wa uaminifu, Bali ni yule aloe na IMANI na MUNGU mwenye dhamiri safi na nia njema mbele za MUNGU.
Mithali 25:19 (KJV) Kumtumaini asiye mwaminifu wakati wa taabu Ni kama jino lililovunjika, au mguu ulioteguka.
MTU ASIYE MWAMINIFU HATUMAINIKI WALA HATEGEMEKI, HATA YEYE MWENYEWE HAWEZI KUJITUMAINIA, HUSEMA HAYA KESHO NITAFANYA LAKINI MOYONI MWAKE ANAJUA KABISA HANA UHAKIKA WA KUFANYA, SI KWASABABU HANA NAFASI BALI KWASABABU HANA IMANI. KINACHOTUSUKUMA KUFANYA VITU NI IMANI, HII NDO SABABU IKIPUNGUA UAMINIFU HUPUNGUA PIA.
Ili kujenga uaminifu wako kwa MUNGU na kwa watu unapaswa kujenga IMANI kwa MUNGU kwanza.
Mithali 29:14 (KJV) Mfalme awahukumuye maskini kwa uaminifu; Kiti chake cha enzi kitathibitika milele.
Itaendeleaaaa usikose sehemu ya tatu
Imeandaliwa na
Emanuel Israel Kangala
@September 2023
No comments:
Post a Comment