LEADERSHIP MENTALITY…
Hapa taongelea leadership kama zao la maono.
Hivyo basi kila unapoongelea uongozi ni wazi kwamba huwezi acha kuongelea maono. Vitabu na Makala nyingi sana zimeandikwa kuhusu uongozi, wasikilize wao, nisikilize pia, then make your own mind.
Kiongozi anahamasishwa na maono aliyonayo, Huku anaewaongoza wanahamasishwa na yeye. (A leader is influenced by his vision, while the follower are influenced by the leader.)
Kinachompa nguvu kiongozi yeyote ni MAONO aliyokuwa nayo. Sababu ya kuanza aliyoanza. Na picha Kubwa anayoiona ambayo inawezekana wengine hawaioni hivyo.
Maono ndio yanayomuamulia ajiri watu wa aina gani, ndio yanayompa nguvu ya kuendelea mbele katikati ya changamoto anazokutana nazo. Imani Kubwa aliyokuwa nayo kiongozi juu ya maono aliyonayo ndio itakayomsaidia kutokukata tamaa katikati ya changamoto.
Kiongozi anapaswa aamini kwenye kile anachokiona zaidi ya MTU yeyote yule.
Imani yake juu ya maono yake ndio yatakayompa kushinda uvivu na changamoto atakazokutana nazo.
Kitu cha pekee kinachowapa watu kushinda uvivu ni msukumo unaotokea ndani yao (maono) au kwa viongozi wanaomwongoza. Bidii nyingi tunazoziona kwa watu huwa zinakuja na matarajio.
Yeyote anaepambana anaamka asubuhi na mapema kwenda kazini anatarajia matokeo Fulani baada ya mda Fulani. PESA, MAONO NA UMAARUFU HIZI NDIZO NGUZO ZINAZOWAFANYA WATU WAFANYE MAMBO YAO KWA BIDII, MAANA WASIPOTIA BIDII WANAONA WAZI KUWA ITAATHIRI YALE WANAYOYATEGEMEA.
Maono huvuta watu na maono huondoa watu, ukiyaasi maono waliovutwa na maono yako huondoka na waliondolewa na maono hurejea.
Maono humjengea mtu tabia na kumuondolea tabia ambazo hazilandani na maono aliyokuwa nayo. Mtu akiyaasi maono tabia zilizoondoka hurejea na zilizojengwa huondoka.
Maono humjengea mtu mipaka na namna ya kuhusiana na watu. Mtu akiyaasi maono mipaka iliyojengwa na maono huondoka.
Msukumo wa kuyafikia maono yako ukiondoka, uvivu hurejea tena, Msukumo ukirudi uvivu huondoka. (ili kuondoa uvivu amsha msukumo mpya ndani yako.)
Maono huvuta watu wa aina mbili wale wanokuja kusapoti na kuhakikisha maono uliyokuwa nayo yanakuwa halisi na kuna wale wanaokuja kwasababu wanaona watajipatia masilahi binafsi kwenye maono uliyonayo kwa muda huo au baadae. Ila wako watakaokufuata sio kwasababu wanaamini sana maono uliyonayo ila kwasababu wanakuamini wewe uliebeba maono hayo kwasababu ya tabia Fulani uliyoionyesha au mambo uliyowahi kuyafanya yanawaaminisha kuwa unaweza kutimiza na maono uliyowaambia. Hivyo watu huwa hawakufuati wewe kama mtu ila matunda(maono) uliyonayo ndio yanayowavuta. Hivyo kama kiongozi hupaswi kuyaasi maono yako, simama imara kuhakikisha yanatimia.
Maono hujenga tabia na kumjengea mtu mipaka, hivyo unavyolinda na kujali tabia zako na mipaka yako hivi vinakuhakikishia usalama wa maono yako.
Uhusiano wowote wenye malengo hutunzwa na kulindwa kwa tabia pamoja na mipaka mliyojiwekea.
Ukitaka kuiharibu ndoa haribu tabia za wanandoa, pamoja na mipaka yao.
Ukitaka kuharibu kampuni au taasisi haribu tabia za viongozi au wahusika wa kampuni na kampuni au taasisi itaharibika.
Tabia na mipaka ni moja ya viungo muhimu sana vya ujenzi katika kuyaendea maono ya taasisi, serekali au ya mtu.
Usikose sehemu ya pili.
Imeandaliwa na
Emanuel Israel Kangala
Email:- emanuelkangala@gmail.com
Phone number:- 0742859313
No comments:
Post a Comment