THE MIND
POLLUTION
Uchafuzi Waakili
UCHAFUZI WAAKILI (MIND POLLUTION)... 19April2019
Utangulizi
Mind pollution: ni kati ya vitu hatari sana hapa duniani, unashangaa mtu anakusifia leo kesho anakuwa wa kwanza kukupiga mawe. na aliekuwa hakuelewi ndio anaekusaidia.
aina hii ya uchafuzi ndio aina mbaya na ugonjwa mbaya zaidi wa akili hapa duniani kwa maendeleo ya mtu binafsi, taasisi, nchi na dunia kwa ujumla.
Matendo 14:1-3 verse “But
the unbelieving jews stirred up the Gentiles and poisoned their minds against
the brothers.”(translation from English standard version).
Matatizo yote tunayoyaona huwa yaanzia
kwenye akili, kuna kitu nakiita mind pollution au uchafuzi wa akili, kama
ilivyo uchafuzi wa mazingira ni hataria kwa afya ya mwanadamu na viumbe hai ndivy ilivyo mind pollution
(uchafuzi wa akili) ni hatari Zaidi maana ndio chanzo cha uchafuzi na chochote
kibovu na kiovu tunachokiona. Embu tuangalia hiii ni nini? Bibilia inasema nini
juu yah iii?
Uchafuzi Wa AKILI (Mind pollution)
ni nini?
Uchafuzi wa akili Ni kuwepo kwa taarifa ambazo
sisahihi kwenye ufahamu au akili ya MTU. Taarifa hizi huanza kubadilisha
namna ya MTU anavyowaza anavyofikiri
na hata namna ya kuongea na matendo yake
huanza kubadilika kwa namna ambae hata yeye anaweza asitambue kwamba
ameanza kutoka kwenye mstari uliosahihi. Mabadiliko haya yanaweza
kuchukua miaka kadhaa kwa MTU
kubadilika kabisa. Hapa ndipo naweza ukashangaa kukutana na MTU ambae alikua anachukia kitu Fulani na kukipiga
vita lakini Leo anakifanya na kukitetea kwamba ni sahihi. Mfalme sulemani
aliangukia kwenye mtego huu. Mtu ambae alipinga sana ibaada za
sanamu mwisho moyo wake unageuzwa wakatiwa uzee wake na kuanza
kuabudu sanamu.(1falme 11:1-3). Mind pollution (uchafuzi wa akili)
ni hatari sana kuliko unavyofikiri. Maana hii
Haijali mtoto, kijana wala mzee, wala haijali
unahekima au la.. karibu tujifunze pamoja
Uchafu ni nini?
Uchafu ni taarifa yoyote ile ambayo IPO kinyume na taarifa sahihi. (kweli). Huo ni uchafu.Taarifa yeyote ambayo haichangii chochote kile
kwenye maendeleo yako ya kiuchumi, kijamii na kiroho huo ni uchafuzi.Umbea, kusengenya, nakusikiliza chochote kile
ambacho akikusaidii kukua kwenye Nyanja hizi nne muhimu yaani kiafya, kijamii,
kiroho na kiuchumi huo ni uchafuzi.
Taarifa zozote zile ambazo zinabomoa
ndoa yako huo ni uchafu.Taarifa yoyote ile ambayo inakuvunja moyo au
kukutia hofu kwenye jambo la msingi unalotaka kufanya huo nao ni uchafu. Taarifa zozote zile zinazokutenga
na Mungu, huo nao ni uchafu, haijalishi amesema nani,
umeangalia wapi, au watu wangapi wanasapoti. Vijana wengi wamearibika kwasababu ya uwepo Wa
taarifa nyingi ambazo ni hasi, watoto
wanaharibika na kuwa na tabia mbaya kwasababu ya taarifa mbaya anazopata kupitia muvi, mziki, YouTube
na n.k.Taarifa za kweli pekee ndizo zinazoweza kumfanya
MTU akue vizuri na awe mwenye furaha
na mafanikio kwenye Nyanja zote.
JE TATAMBUAJE TAARIFA ZA KWELI?
Mwenye taarifa sahihi ni
mtengenezaji Wa kitu hicho. Mara nyingi watengenezaji hutoa taarifa ya namna ya kutumia
na kutengeneza chombo hicho ikiwa kimeharibika ijulikanayo kama USER
MANNUAL BOOK. Dunia na vyote viijazavyo vinavyoonekana na visivyoonekana
vimeumbwa na Mungu. Hivyo
MUNGU ndie mwenye taarifa sahihi kuhusu
vitu vyote vya duniani na mbinguni. Mwenye taarifa sahihi
kuhusu wewe na vitu vinavyo kuzunguka ni Mungu Pekee. Lakini pia
Mungu ametupa User Manual (kitabu chenye taarifa sahihi) yaani BIBLIA. Taarifa zozote ambazo zipo kinyume na neno la Mungu au taarifa alietoa
Mungu huo niuchafu..1 Wakorinto:10.26, Mwanzo1:1, zaburi24:1.Lakinipia fahamu hilikila kitu
kimetengenezwa kwa kanunina iliupate matokeo ulio haidiwa nilazima ufuate kanuni,
na kanuni hizo ni moja ya taarifa sahihi ambazo zinapatikana kwa mtengenezaji
pamoja na User Manual (kitabu chenye Maelezo ya namna ya kutumia
na taarifa zote za muhimu) alietoa.
Na
ukienda kinyume na taarifa alie toa mtengenezaji kamwe huwezi kupata
matokeo aliyokuahidi.
Pia fahamu hili taarifa yeyote yenye ukweli
asilimilia 99% na uongo 1% uwe na uhakika hizo taarifa siyo sahihi.Kama
nilivyosema mwanzo kila kitu kimetengenezwa kwa kanuni hivyo ukivunja
kanuni hata moja huwezi pata Matokeo yaliokusudiwa na hii Ndio sababu
Biblia inasema ukivunja sharia moja umevunja zote maana kanuni zote zipo
kwenye hicho kitu kimoja na zimewekwa
na mtengenezaji. Yakobo2:10
Mfano:
Siku moja nikiwa napita maeneo Fulani nilikuta
sehemu moja wana uza taa za umeme. Kwa Maelezo yamuuzaji taa hizo zina
tumika kwenye umeme Wa nyumbani ujulikanao kama UMEME WA TANESCO. Basi nikachukua taa
hiyo na kwenda Nayo nyumbani, nilipofika
niliiweka taa hiyo na kuwasha swichi yangu ya umeme. Baada ya kuwasha tu swichi
taa ile ililipuka SAA hiyo hiyo. Haraka nikachukua kasha ambayo iliwekwa humo
ilikuangalia maelekezo ya mtengenezaji, nilipoiangalia nikagundua
ilikuwa ni taa ya solar volt12, na Mimi nimeiweka kwenye umeme Wa volt Zaidi
200. Nikaishia kupata matokeo ambayo sikutarajia
FAHAMU HAYA:
1. Hutapata matokeo yaliyokusudiwa na
mtengenezaji kama ukivunja kanuni mojawapo
ya zile alizoziweka kwasababu zozote zile hata kama hahukujua, ulidanganywa au hakupata taarifa zote.2.Taarifa zote unazopewa uwe na mazoea ya
kizipima na taarifa ya mtengenezaji(
usermanual).
Kwanini uzipime?
Mtoa taarifa anaweza akawa anaangalia
maslahi yake bila kujali matokeo utakayopata.
Au Amesahahu au hakuelewa vizuriau hakusoma
kabisa taarifa ya mtengenezaji
na anatumia uzoefu kutokana na vile alivyosikia au kufundishwa. Weka hii akilini kila taarifa unayopewa ipime
na taarifa ya mtengenezaji. Vinginevyo
utamlalamikia mtengenezaji kwa kupata matokeo hasi (negative) kwa uvivu wako Wa
kutokusoma taarifa alizozitoa.
Fahamu ili.
Taarifa zote muhimu za
kukuhusu wewe na vitu vinavyokuzunguka vinapatikana
kwenye BIBLIA ambayo ndiyo user manual tuliopewa.. Usiiamini taarifa yeyote inayopingana na Neno
la Mungu yaani Biblia.. Hata kama inatoka
kwa kiongozi Mkubwa na unaemwamini sana. Usimwamini MTU yeyote kupita unavyo mwamini Mungu.Uwe na tabia ya kuisoma Biblia yako ili uweze
kupambanua taarifa sahihi na ile isiyo sahihi.
VYANZO VYA TAARIFA
Taarifa zote sahihi na za kweli
zinatoka kwa Mungu pekee na si kwingineko Chanzo cha taarifa zote za uongo ni shetani na
yeye ndie baba Wabongo. Lengo
lake kubwa ni kuharibu na kutuweka mbali
na Mungu ili aweze kutuchezea,
kutuharibu na kutuangamiza kabisa.
Fahamu ili.
Pia ana uwezo Mkubwa Wa kumshawishi na kumdanganya
MTU iliafuate uongo wake
hasa asiekuwa na hiyo kweli ya Mungu.
Na ndomaana hata Yesu mwenyewe alivyojaribiwa
alimshinda Kwaneno (kweli) ya Mungu
Taarifa unazoangalia you tube, muvi
unazoangalia, mziki, majarida unayosoma,genge
unalokaa, maarifiki ulokuwa nao, Je wanakujenga au wanakuboa kwa taarifa zao? Kwasababu shetani huwekeza kwa MTU taarifa hasi
na Mungu huwekeza taarifa chanya kwa watu
pia,hivyo kuwa maakini na hadithi mnazo piga pamoja na taarifa unazopata.
NAMNA YA KUJILINDA NA MIND POLLUTION: Biblia imeweka wazi namna yakuepuka tatizo hill.
Hata kabla ya mfalme sulemani Mungu alitoa mausia juu ya hili. Hebu
tuangalie mistari michache ya Biblia Mungu
aliwaambia wana Wa Israeli wasioe MTU Wa mataifa wasije wakageuzwa mioyo yao ielekee Baali.(Kumb7:2-5,kumb17:14-20)Sulemani
pamoja na hekima alivunja mausia haya na mwishoni
moyo wake uligeuzwa na kuanza kuabudu miungu
mingine.(1falme11:1-3)Hii inaonyesha wazi Mungu alifahamu nguvu ya taarifa unazozipata
kila siku zinauwezo Mkubwa Wa kumbadilisha MTU haijalishi anamfahamu
Mungu kiasi gani au ana hekima kiasi gani.Lazima uifahamu kweliYesu akasema mtaifahamu kweli na hiyo kweli itawaweka
huru. Kuwa na taarifa sahihi kutakupa uwezo
Wakupambanua taarifa za uongo. Taarifa yenye ukweli asilimia99% na uongo asilimia1%
inahitaji MTU mwenye uelewa Mkubwa juu ya hiyo kweli ilikubaini uongo huo,
na kujua kua taarifa hiyo si sahihi. Na hii Ndio sababu Mungu akatupa user
manual (Biblia) ili kila taarifa
1.tunayoipata tuipime kwa hiyo. Sasa hutaweza
kupima kama huifahamu hiyo kweli.Weka kila jitihada kuifahamu kweli
yaani neon la Mungu (Biblia).
2.Ufuate mausia ya Mungu.
3.Usiketi baradhani pawenye midhaa..
Zaburi1:1-
4.Uwe na marafiki mwenye hekima
(wazuri).
5.Soma na kulitafakari neon la
Mungu. Yoshua1:8
6.Tafakarini mambo yoyote yaliyo mema.(Filipi4:8,
Efeso4:16)
7.Kesheni mkiomba...Luka11:36
MADHARA YA UCHAFUZI WA AKILI.
(MIND POLLUTION) Taarifa zote ambazo ni hasi zinakutoa kwenye
kweli na kukuingiza kwenye hatia. Taarifa
hizi huzuia mafanikio ya mtu katka Nyanja zote.
Fahamu hili
hatma ya taarifa hasi (mind pollution) ni mauti.
Kwa Mara ya kwanza mind pollution ilitokea pale
bustanini mwa edeni, baada ya hawa (Eva) kuziamini taarifaa mbazo ziko kinyume
na zile alizotoa Mungu. Hapa ndipo chanzo cha mwanadamu kutenda kinyume
na Mungu. Na Mara nyingi taarifa hasi zinaweza kuja na ahadi nyingi
ambao mwisho wake ni mauti. Adamu na Hawa walipoenda kinyume na taarifa alietoa
Mungu hawakupata Yale
matokeo ambayo shetani aliwaambia Bali Yale ambayo Mungu aliwaambia.(hakika mtakufa).Wana Wa Israel walipoenda kinyume na taarifa
alizotoa Mungu waliangukia utumwani.
Paulo akasema sisije tutapataje kupona tusipojali
wokovu mkuu namna hii? Luka:13.3 Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu,
ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo.
Ezekieli:18.4 Tazama, roho zote ni mali yangu;
kama vile roho ya baba ni mali yangu, ndivyo ilivyo roho ya mwana mali yangu; roho ile itendayo dhambi itakufa. Nimalizie Kwa kusema hivi wale waliotumwa kuipeleleza
yeriko kati ya watu kumi na mbili
ni watu wawili tu walioleta taarifa njema ila kumi wote walileta taarifa mbaya mbele ya wana Wa
Israel na mwisho wana Wa Israel wa kaamini taarifa za wale kumi ambazo zilikuwa kinyume na Mungu, hata ikazua ugomvi na watu wengi kupoteza maisha na kushindwa kufika kule
ambako Mungu alikusudia kuwafikisha. Kuna
wakati mwingine hatujafika mahali ambako Mungu amekusudia kiuchumi ,jamii, kiroho hata kimwili kwasababu ya mind
pollution(taarifa hasi tulizopata na kuziamini). Weka bidii ya kutafuta na kuamini
taarifa za kweli.
NAMNA YA KUONDOA ATHARI ILIYOSABABISHWA
NA UCHAFUZI WA AKILI:Cha kwanza ambacho ni muhimu ni lazima uondoe
kwanza taarifa zote ambazo sisahihi zilizoleta madhara kwenye maisha
yako. Nakuzireplace na taarifa sahihi. Lakini pia tambua hili:-
Taarifa hasi ni rahisi sana kumwingia mtu na
kuacha athari kwenye maisha yake. Kama
ilivyo ni rahisi kuchafua kuliko kusafisha.
Ningumu sana kwa taarifa hasi kuondoka, inahitajika
gharama, kama ilivyo kusafisha ni gharama,
pia kusafisha akili, kuondoa huo uchafu kwenye akili kuna gharama.
Chagua kuziamini, kuzitii na kuzifuata taarifa
za Mungu bila kujali wengi wanasema
nini. Kisha,..
1.Kaa mbali na vyanzo vya taarifa
hasi,
2.Fanya bidii kusikiliza, kuangalia
au kusoma taarifa sahihi, zitafakari na kuziamini
Mind pollution inamplekea mtu kutenda dhambi,
na dhambii na mtenganisha mtu na Mungu.Yesu alikufa msalabani ilikurudisha kutupatanisha na Mungu, maana uhusiano wetu uliharibiwa na dhambia
mbayo chanzo chake ni baada ya adamu na Haaa kuamini taarifa hasi zilizoletwa
na shetani. Ashukuriwe Mungu kwamaana Kwa kumuamini Yesu
kristo madhara yote na vifungo vyote vilivyosababishwa na mind pollution
zina safishwa na kutuacha huru kabisa. Huku tukivikwa uwezo Wakuishi sawa
sawa na makusudi ya Mungu.
Maisha yenye furaha na mafanikio halisi yanapatikana
ndani ya wokovu. Fanya maamuzi sasa.Maisha bila Mungu ni sawa na chai yenye viungo
vyote karafuu, iliki, n.k lakini ikakosa sukari. Hakika nakuambia hatakama inanukia kiasi gani hainyweki ukipeleka mdomoni utatema tu. Ni sawa na maisha ya mtu
mwenye kila kitu akamkosa MUNGU.
Lakini pia kumbuka chai ni nzuri inapokuwa ya
moto ikipoa tu hau taweza kuitumia, ndivyo ilivyo Kwa maisha ya mtu alieokoka,
uliitwa na kusafishwa ukaokolewa ilipia uwe mtakatifu kama Baba (MUNGU)
alivyomtakatifu. Kuna wengine hawaeleweki mambo wanayofanya, wengine
wanaangalia X na mambo mengi ambayo hata katika jamii tu hayafai.
Wengine wanavaa mavazi ambayo hata jamii inashindwa kuwaelewa, wamekuwa
kama chai iliyopoa hainyweki sasa ndungu yangu sibora
ungebakikuwa Maji maana Maji ya baridi yananyweka vizuri.
Iliuendelee kuwa moto hakikisha
unasoma na kutafakari Biblia, unaomba Mara
tatu Kwa siku, na kufunga angalau Mara moja Kwa wiki na kuyaishi Yale ambayo Mungu anasema na wewe.Kama unapata shida kwenye usomaji Wa Biblia.
Unaweza kujiunga na magrup mbalimbali yatakayokusaidia kujisomea Biblia yako mwenyewe.
Kama BIBLE RACE2 019, NA Gospel unlimited
fellowship
Imeandaliwa na
Emanuel Israel kangala
+255742859313
Baruapepe: emanuelkangala@gmail.com
19April2019
No comments:
Post a Comment