UNACHOKITAFUTA SICHO ULICHOKIPOTEZA. - EMAGK SITE

Latest

This website was designed to help college student especially those who takes engineering course for review, past paper and other learning material. And teacher for review.

Wednesday, November 24, 2021

UNACHOKITAFUTA SICHO ULICHOKIPOTEZA.

 


UTANGULIZI.



Ili kuwa na ushawishi na mafanikio makubwa na kuishi maisha ya utoshelevu hapa duniani ni muhimu sana kukipata kile ulichokipoteza. Asilimia kubwa ya watu hapa duniani tunachokitafuta sicho tulichokipoteza, na ndomaana utoshelevu na maisha ya furaha yamekuwa adimu sana kwa wengi. Na wengi waliogundua siri hii na kujua walichokipoteza na wamebahatika kupita njia sahihi na kukipata walichopoteza wanaishi maisha ya mvuto huku wengine tukila matunda yao bila kujua siri iliyo nyuma ya mafanikio na utoshelevu wao.

 

Nimatumaini yangu baada ya kuijua siri hii, utachukua hatua madhubuti katika kutafuta na kudumu ili kuishi maisha yenye mafanikio na utoshelevu tele.

 

Tuanze pamoja kuivumbua siri hii.

 

SEHEMU 1: SOMETHING IS WRONG:-

Kila kitu Duniani hutengenezwa kwa kanuni maalumu na ili kitu hicho kifanye kazi ipasavyo, nilazima kanuni hizo zifuatwe.

The best performance of your tools depend on how you handle them by following the manufacturer instruction.

Mtu alitengenezwa afanye kazi kwa ufanisi kwenye kanuni na mazingira Fulani. Matokeo ya maisha kuwa magumu, na uonevu wote tunaouna ni matokeo ya kutokufuata kanuni zilizowekwa. Au kuacha kanuni/maelekezo moja kati ya zile zilizowekwa/kutolewa na Mtengenezaji.

Sasa ivi ukiangalia kwa makini unashindwa kuelewa kipi ni bora hapa Dunia, Which button to press  inorder to get and live a happy life.

 Is it wealth?, If it’s the wealth, why wealth people they depend on witch doctors that in turn they are not wealth like them. Wengine mahusiano yanawazingua mpaka unashindwa kuelewa kipi ni kipi? Wakati wako wanoamini mahusiano yao yanayumba kwasababu hawana pesa.   Kipi ni kipi?

Or is it  Education?

But we see most of educated people support stupid things that actually you feel like no. Nawasomi wengi pia wanaenda kwa waganga wakienyeji wasiokuwa na elimu hata ya darasa la saba ili wapate kazi, wapande vyeo au wadumu kwenye nafasi/ajiraa zao. Kipi ni kipi.

Or is it Position? Au nafasi ya kiuongozi?

Lakini kuna viongozi wanaoenda kwa waganga wa kienyeji au viongozi wa dini ili wadumu au wapate nafasi za uongozi. Which is which?

Umaarifu ndo umekua harufu ya uvundo wa uovu kwa wengi.

Kuna kitu hakijakaa sawa na kwambia.

 

THE IMPORTANT LINK:

Ukiangalia kwa makini utagundua kitu, Watu wenye pesa (matajiri), wasomi, wenye vyeo na watu maarufu wote kwa namna moja ama nyingi kufanikiwa kwao na kutunza nafasi zao wamewahusisha eidha viongozi wa dini au waganga wa kienyeji (huwa nawaita watu wenye uwezo wa kuwasiliana na Ulimwengu wa Roho, ilikuleta majibu katika ulimwengu wa mwili).

 

Watu hawa hawajafanikiwa kama wao, hawana umaarufu au nafasi kama zao, lakini huwategemea wao ili kupata na kudumu katika nafasi zao au utajiri wao.

 

Katika kutafakari kwangu nikagundua, mwenye million anafikiri akiongeza utajiri wake na kuwa millionea basi atakuwa ameipata furaha yake lakini akifikia kiwango hicho anajikuta bado ni mtupu na hana furaha na Amani ya moyo Bali woga na wasiwasi wa kufeli unamtawala hivyo hufikiri labda akiongeza utajiri wake kidogo Basi atakuwa na furaha lakini wapi, vivyo hvyo kwenye cheo na umaarufu.

Hii Inanipa picha kuwa kama ilivyo chai hata ikiwa na viungo vyote lakini ikikosa sukari hainyweki, ndivyo ilivyo kwenye maisha yetu kuna kitu cha msingi ambacho hicho kikikosekana maisha hayana ladha.

 

USITEGEMEE FURAHA YAKO ITALETWA NA VITU FULANI, LA HASHA FURAHA IKO NDANI YAKO, KAZI YAKO NI KUKAA KWENYE MAZINGIRA SAHIHI.

 

SEHEMU 2

Samaki aliumbwa ayafurahie maisha akiwa majini, ukimuweka nchi kavu hakika atateseka na mwisho atakufa.

Fahamu ili kila kitu MUNGU alikifanya kifanye kazi vizuri kwenye mazingira Fulani. Kama ilivyo meli ilitengezwa itembee kwenye maji ukiiweka nchi kavu haiwezi hatakama ina injini kubwa Zaidi ya injini ya gari, kwasababu si mazingira yake.

 

Ukimpeleka nyani aishi baharini, hataweza kwasababu hayo si mazingira yake. Yeye ameumbwa kuyafurahia maisha nchi kavu, kwenye miti yenye matunda na mizizi inayomfaa.

 

Ndivyo ilivyo Mwanadamu aliumbwa ndani ya uwepo wa MUNGU, maisha ya mwanadamu yanakosa ladha nje ya uwepo wa MUNGU.

Kama ilivyo mkimchukua swala na kumfuga kama mbuzii wa kisasa na ukampatia kila kitu, hawezi kuwa na furaha hadi kufa kwake, tatizo si majani bali mazingira, yeye aliumbwa ayafurahie maisha huko porini.

 Ndivyo ilivyo, elimu, mali, umaarufu wala cheo haviwezi kumpa mtu furaha nje ya uwepo wa MUNGU. Elimu, mali, umaarufu vyote hivi huwa na maana mtu akiwa ndani ya uwepo wa MUNGU. Maana haya ndiyo mazingira ambayo mwanadamu alitengenezewa ili ayafurahie maisha siku zote. Na hii ndo maana wenye elimu, maarufu na cheo huenda kwa watu wenye uwezo wa kuwasiliana na ulimwengu wa roho ilikuleta majibu kwenye ulimwengu wa mwili (waganga wa kienyeji, viongozi wa dini, mitume, manabii n.k) ili kupata kazi au kudumu kwenye nafasi zao.

 “Mali, umaarufu na cheo nje ya uwepo wa MUNGU havina ladha ni sawa na chai yenye viungo vyote lakini ikakosa sukari.”

 

“Kuweka juhudi katika kutafuta mali, pesa, umaarufu na vyeo huku ukimsahau au kumuacha MUNGU ni sawa na kujiponya na chui anaekukimbiza porini kwa kupanda juu ya mti. UTAKUFA.”

 

 

 

SEHEMU YA 3:  NINI KIMETUFIKISHA HAPA TULIPO:

Je nini kimetufikisha hapa kuamini kwamba elimu ni ya muhimu kuliko vyote lakini baada ya kupata elimu, tunaenda kwa waganga wa kienyeji au kuombewa ili tupate kazi, inamaana elimu imeshindwa kutatua tatizo hilo? Tunawaacha wapi wenye vyeo na mali, watu maarufu je?

 

Ukimweka nyani bahari atapambana kutoka kwenye maji iliarudi nchi kavu kwenye mazingira yake ya kujidai, anaweza akafa kabla ya kufika nchi kavu au akafika nchi kavu akiwa amechoka.

Vivyohivyo samaki pia ukimweka nchi kavu atapambana arudi baharini, ila bila msaada itakuwa ni ngumu sana kurudi baharini, kwasababu mazingira aliyokuwepo hajayazoea na hawezi kuyamudu kutokana na maumbile yake.

Ndivyo ilivyo kwetu sisi, Baada ya adamu kupoteza uwepo wa MUNGU tumekuwa tukiangaika huku na kule kurudi kwenye mazingira tuliyoumbiwa ili tuyafurahie maisha.

Baada tu ya kupoteza uwepo wa MUNGU ambayo ndiyo yaliyokuwa mazingira sahihi ya mwanadamu kuishi, mwanadamu alianza kujithaminisha na vitu. Kama mali, umaarufu na Elimu.

Mtu mwenye elimu kubwa alionekana wa thamani sana kuliko yule ambae hana, na Mtu mwenye cheo na umaarufu hawa walithaminiwa sana kuliko wale wasiokuwa na cheo wala kujulikana. Sumu ikawainazidi kuenea hata hivi leo.

Sumu hii ilipandwa na shetani pale kwenye Bustani ya Edeni.

 

Nikukumbushe kitu, Thamani ya dhahabu haishuki kwasababu imefunikwa na matope Bali thamani yake huonekana baada ya kuoshwa na kuchongwa vyema. Ndivyo ilivyo thamani yetu haishuki wala kupanda kwasababu ya elimu, cheo au umaarufu, Bali vitu hivi vinaweza kutumika kuionyesha thamani yetu kwa wengine.

FAHAMU HAYA:

Hatusomi ilituwe bora au na thamani kuliko wengine la! Bali tunasoma ili tuje kuwatumikia wengine kwa ujuzi tutakaoupata.

 

Hatutafuti vyeo ili tuwe na thamani na kuwadharau wasionavyo la hasha! Tukiwa viongozi ni kwasababu tumeaminiwa Kuwa tunaweza kuwatumikia wengine vyema kwenye nafasi hizo.

 

Elimu, umaarufu au cheo Kisikufanye uwadharau au kuwaonea wengine.

 

Thamani ya dhahabu haishuki kwasababu imefunikwa na matope Bali thamani yake huonekana baada ya kuoshwa na kuchongwa vyema, Ndivyo ilivyo dhambi na tabia zote mbaya ufanyazo zinaweza kufunika au kuficha vipawa, uwezo, karama na thamani halisi ambayo Mungu aliiweka ndani yako.

VIVYO HIVYO kama DHAHABU kubali kuoshwa na kuchongwa ili thamani yako ionekane hata kwa wasiokufahamu.

 

SEHEMU YA 4:

Kama ilivyokawaida Samaki akitoka kwenye maji au bahari na kuingia nchi kavu anahitaji msaada ili aweze kurudi baarini. Kwasababu kuona kwake, kutembea na mtazamo wake huathiriwa na mazingira hayo mageni.

 

Ndivyo ilivyo kwetu sisi baada ya kupotea, tulihitaji msaada maana mtazamo wetu, kuona kwetu uliathiriwa na mazingira hayo mageni nje ya uwepo wa MUNGU, Bila msaada tunaweza kufika kwenye mazingira hayo kwa kuchoka au tukafia njiani. Hivyo msaada wa MUNGU ulikuwa wa Muhimu sana ili kurudi kwenye uwepo wake.

 

Utaratibu ulifanyika na msaada ukapatikana, MUNGU akatupa njia na uwezo kupitia YESU KRISTO ili turudi kwenye uwepo wa MUNGU, na kuyafurahia maisha.

Kazi ni kwetu ya kukubali msaada huo, kwa kumkiri kuwa ni BWANA na MWOKOZI wa maisha yetu ili kurudi kwenye uwepo wa MUNGU.

Na hii ndio sababu wote waliokubali msaada huu wanafurahia maisha wakiwa na pesa au hawana, wenye cheo na wasionacho. Kama vile chai ikikosa viungo vinavyoifanya inukie lakini ikawa na sukari na majani basi itanyweka bila shida. Lakini ikikosa sukari haiwezi nyweka.

 

Mali umaarufu na vyeo havina maana kama hutakuwa na uwepo wa MUNGU kwenye maisha yako.

 

Tafuta na udumu kwenye uwepo wa MUNGU ili uyafuruahie maisha. Na hiii ndo sababu wenye elimu huenda kwa waganga wa kienyeji ambao hata hawana elimu kama yao lakini wanauwezo katika Roho.

Jijenge katika MUNGU, Usiache kung’ang’ana na kuendelea kudumu kwenye kanuni za MUNGU Ili kuongeza uwezo wako wa KIROHO.

 

JICHUNGUZE, JITAFAKARI? TULIPOTEZA UWEPO WA MUNGU NA MAHUSIANO YETU NA MUNGU YALIHARIBIKA. TUNAPASWA KURUDI KWA MUNGU.

 

 

 

KUJUA ULICHOPOTEZA NI JAMBO MOJA, KUIFAHAMU NJIA YA KUPITA NI JAMBO LINGINE.

Ni muhimu tufahamu pia kujua tulichopote ni jambo moja ila tuna takiwa pia tujue njia sahihi ya kupita ili tufike au tupate tulichikipoteza.

Tumeshafahamu kuwa tulipoteza uwepo wa MUNGU maishani mwetu, ushirika na MUNGU, au kwa maaana nyingine uhusiano wetu na MUNGU uliharibika baada tu ya kutenda dhambi. Ok sababu ya kuvunjika kwa uhusiano wetu na MUNGU ni dhambi. Basi ukiangalia kwa makini unaona kilichotutenga na MUNGU na kuondoa uwepo wake kwenye maisha yetu ni dhambi.  Ok kwahiyo tunachotakiwa kufanya ni kuondoa dhambi kwenye maisha yetu na kurudisha uwepo wa MUNGU.

 NINI TUFANYE ILI KURUDISHA UWEPO WA MUNGU MAISHANI MWETU?

Njia pekee ambayo MUNGU alitupa ya kutupatanisha sisi na YEYE ni YESU Kristo. Alikufa msalabani kwaajili ya dhambi zetu. Alibeba  adhabu iliyokuwa juu yetu kwa huruma na upendo mwingi alistahimili kifo cha msalaba ili sisi tupate kupona.

Ila kama ilivyo Mungu sio Dikteta anataka kila mmoja aamue kwa dhati kumfuata na kuishi ndani yake ili ayafurahie maisha.

Kazi yetu ni hii tu Marko 16:16:- Aaaminie na kubatizwa ataokoka, kazi yetu kubwa ni kuamini tu.

 

Kama bado hujamwamini YESU kuwa BWANA na mwokozi wa maisha yako, Muda ni sasa.

OMBA MAOMBI HAYA PAMOJA NAMI

MUNGU MUUMBA MBINGU NA NCHI, NASHUKURU KWA UPENDO WAKO WA AJABU KWA KUMTOA MWANAE YESU KRISTO KUFA MSALABANI KWAAJILI YANGU. NINAMWAMINI YESU KRISTO NA KUMKUBALI KUWA BWANA NA MWOKOZI MAISHA YANGU. KARIBU YESU UFANYE MAKAO NDANI YANGU. KUAANZIA SASA NINAKUKABIDHI MAISHA YANGU, NIMEDHAMIRIA KWA DHATI KUYAISHI NA KUENENDA SAWASAWA NA NENO LAKO. KWA JINA LA YESU KRISTO NINAOMBA AMEEN.

Sasa umeokoka, unaweza kuwasiliana nami kwa msaada Zaidi

Kwa namba 0742 – 859-313 au email: emanuelkangala@gmail.com

Au tembelea kanisa lililokaribu nawe kwa msaada Zaidi. (WEWE NI WA THAMANI SANA.)

 

Tambua Shetani “Anaweza kukushawishi na kukuambia uzuri wa ubaya au uovu wowote anaotaka uufanye huku akificha nia yake ovu ya kuua na kuharibu.”

Lazima Tutambue kuwa mshahara wa dhambi ni mauti, haujawahi kubadilika, na hautakaa ubadilike, Mwanzoni utakuvutia na kuona unafaida lakini mwisho wake ni majuto na mauuti ya milele.

Warumi 6: 23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, Bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo YESU Bwana wetu.”

 

Yohana 14:6:- YESU akawaambia, mimi ndio njia na kweli na uzima, mtu haji kwa baba, ila kwa njia ya mimi.

Marko 16:16:- Aaaminie na kubatizwa ataokoka, asie amini atahukumiwa.

Mathayo 6:33 “Bali utafuteni kwanza ufalme wa MUNGU na haki yake na hayo mengine yote mtazidishiwa..” (Cha kwanza uwepo wa MUNGU, mengine yote utayafurahia ukiwa ndani ya uwepo wa MUNGU.)

 

Mathayo 22:37 Akawaambia mpende Bwana MUNGU wako kwa Moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.

Soma pia Marko 12:30, Luka 10:27, kumbukumbu 6:5, kumbukumbu 11:1, kumbukumbu 6:5.

IMEANDALIWA NA:-

               Name:- EMANUEL ISRAEL KANGALA

                  Phone no:- 0742-859-313

                 Email: emanuelkangala@gmail.com

               Website: emaisra.blogspot.com

 

No comments:

Post a Comment