USIFE KIBUDU - EMAGK SITE

Latest

This website was designed to help college student especially those who takes engineering course for review, past paper and other learning material. And teacher for review.

Tuesday, April 26, 2022

USIFE KIBUDU

BADO TUMAINI LIPO.

HEKIMA ZA MZEE 2060'S



UTANGULIZI:

Makala hii imeandikwa kwa namna simulizi ilikuwa rahisi pia kwa kila mmoja kuisoma na kujifunza baadhi ya vitu nilivyoona ni vyamuhimu sana kushirikiana na wewe kwa njia hii, ambazo zitatusaidia kukua kiuchumi, kijamii, kiroho na kwenye Nyanja zote za maisha yetu.

Enjoy as you Read.

Umebarikiwa sana.




SEHEMU YA KWANZA.

Ilikuwa majira saa kumi na mbili jioni wakati wa jua kupunga, nikiwa kwenye kilima kimoja maarufu kijulikanacho kwa jina la mlima NGANGU, kilichopo kilema marangu. Kulikuwa na mandhari nzuri sana na muonekano mzuri wa kilele cha mlima Kilimanjaro. Jua lile la adhuhuri lilifanya mazingira yale kuvutia na kupendeza pamoja na upepo mwanana na hali ya hewa ya ubaridi kabisa.  

Nikiwa nimejilaza kwenye majani na kuendelea kuyapa macho furaha yake huku mwili ukifurahia upepo mwanana na hewa safi inayopatika kwenye eneo hilo.  Nikiwa katika kutafakari kwangu, Ghafla mawazo yangu yalipaa na kunichukua hadi sehemu moja mwanana yenye maji ya ubaridi sana na kijani kizuri kilichovutia macho. Nilisikia sauti ikinitaa, niligeuka ilikuona ni nani alieniita, nilishangaa kumuona mzee mmoja ambaye sura yake haikuwa ngeni sana machoni pangu, nilimuangali kwa mshangao huku mawazo yakijaa atakuwa nani? Na niliwahi kumuona wapi? Wakati nikiendelea kuwaza hivyo, alinisogelea karibu na kunigusa akaniambia, mwanangu kuna mambo machache nataka nikueleze, kwanza kabisa lazima ufahamu kuwa kabla ya kuanza kujua wengine unatakiwa ujifahamu mwenyewe. Ila hicho sicho kilichonileta. Mzee akandelea kusema Huku nikimkazia macho bila kuongea chochote. 

Alinikazia macho kama mtu ahakikishae mtu anaeongea nae kabla ya kuongea ili maneno yake yasianguke bure, 

Mzee akaniambia Mwanangu dhahabu ni njema sana na ni moja ya madini yenye thamani kubwa hapa Duniani, Lakini thamani ya madini hayo haiwezi kuonekana kabla ya madini hayo kuchakatwa. Namaanisha ubora wa madini ya dhahabu hauonekani tu kwasababu ni dhahabu Bali kwasababu ya ubora wa bidhaa yake baada ya kuchakatwa. 

Mzee akaendelea Hivi unakumbuka enzi zile za ukoloni, wazee wetu walitumia dhahabu kuchezea bao, Kwasababu ndio matumizi pekee waliyoyafahamu ya dhahabu, na wazungu walipoingia waliwapa gololi wao wakatwaa dhahabu, Baadae wakarudisha vifaa au bidhaa zilizotengenezwa na dhahabu na kuziuza ghali  sana kwa wazee wetu, naamini kabisa wazee wetu walizifurahia sana bidhaa zile.

Mwanangu Dhahabu haikupoteza thamani yake kwasababu wazee wetu hawakuitambua au kujua namna ya kuitumia, Bali thamani yake ilibaki palepale ila ilikuwa imefichwa machoni pao.

Watu wanaweza wakakukataa, wakakubeza na kukutumia vibaya, hiyo haimaanishi kuwa huna thamani, Bali ni indicator (ishara) ya kwamba unahitaji kuchakatwa ili uwe bora Zaidi, thamani yako ionekane.

Vijana wengi tunakwepa mchakato, tunaogopa kuchakatwa, kumbuka ili dhahabu ili iwe mkufu au heleni au bidhaa yoyote ile unayoijua ni lazima ipitie mchakato, kwanza kabisa itaoshwa na kuondolewa uchafu au wataalamu wanaita impurities ilikubakisha dhahabu safi, Baada ya hapo itachongwa kwa ustadi ili kupata bidhaa inayotakiwa. Bidhaa hizi humvutia kila mmoja anaejua dhahabu au asieifahamu.

Ndivyo ilivyo wewe ni wa thamani sana ila thamani yako imefichwa ndani yako, na ili ionekane unahitajika kuoshwa kama dhahabu, au kuacha tabia zote ambazo hazifai au zitaaribu au kubadili muonekano wa thamani kubwa iliyo ndani yako baada ya kuchongwa.

Huna budi kukubali mchakato, kuchongwa, hapa kuna maumivu ya kila aina ila uvumilivu unahitaji ili thamani kubwa ambayo Mungu ameweka ndani ionekane, watu waifurahie, Jamiii iifurahie.

Mwanangu ni kweli dhahabu hata ikiwa kwenye matope ni dhahabu, hata ukiitupa chooni bado ni dhahabu, ila ili thamani yake ionekane kwa kila mtu anaeifahamu na asieifahamu ni lazima ichakatwe. 

Toka chooni, toka kwenye matope kubali kuchakatwa. Usikae kwenye historia ya zamani, ni kweli ulionewa, ulitendewa ukatili na ni kweli kabisa ulitukanwa na kusalitiwa, ILa toka uko. Usije kufa watu wakijua ulikuwa kuku Kumbe wewe ni Tai. Kubali mchakato uidhihirishe thamani na urudishe heshima yako. Dhahabu inaheshimika bhana.. alaa.

Nilikaa kimya kama mtu aliemwagiwa maji ya baridi, Mzee aliendelea

Ukitaka ujulikane na uwe na faida ni lazima upitie mchakato, Baadae utatoka kama dhahabu, watu wote wanaokufahamu na wasiokufahamu watakufurahia, utasemwa hata na watoto ambao hawajawahi  kuiona sura yako. Kama dhahabu inavyonenwa na kila mtu aliewahi kuiona na asieifahamu kabisa, sifa zake zimevuma hadi miiisho ya Nchi.

Kuna namna mbili ya kufanya ili uketi pamoja na wakuu, namna ya kwanza ni kujipendekeza kwa wakuu. Na uwe na uhakika ukitumia njia hii watakutumia na kukutumikisha kama kibaraka wao. Ila namna ya pili ni kuwa bora kwenye kile kitu ambacho Mungu ameweka ndani yako. Kwamaana ingine ni kutoa ile thamani ambayo iko ndani ioneka nje. Uwe na uhakika hapa hautawatafuta wakuu bali wao watakutafuta wewe.

Kazi ni kwako, matunda yako yataamua yamvute nani.

Mwanangu mti unapendwa kwa matunda yake, Kinachowavutia watu kwenda kwenye mti Fulani ni matunda au matumizi ya mti huo. Kitakachowavuta watu ni matunda unayotoa, au faida wanayopata kwako. Pia kitakachowafanya wadumu pamoja na kukufurahia ni kudumu kwa matunda unayoyatoa. Watu hurudi nyuma pindi wanapokosa walichokifuata. Hivyo unapaswa kuwa bora kila iitwapo leo. Wasije wakakukata na kukuondoa katika nchi, maana kama huna matunda hata nchi unaiharibu.. Hahahahaha hapa mzee aliangua kicheko kidogo.

Alafu akaniambia wakati mti unapambana kuzaa matunda watu hukaa mbali wala hawahusiki kwa chochote ila yanapozaliwa matunda watu huusogelea mti ili kula matunda yake. Ndivyo ilivyo wakati unapambana  watu wataonekana kuwa mbali na wewe, Ila baada ya matokeo kila mmoja atakutafuta na kukufurahia, usishangae utawafahamu ndugu wengi ambao hukuwafahamu mwanzo. Haya ndo maisha yalivyo mwanangu wala usije ukawachukia.

Kumbuka hauna maana hapa Duniani kama huna matunda, si unakumbuka YESU aliwahi kutoa mfano wa mti uliokuwa unatunzwa lakini hauna matunda, Mwenye shamba akamwambia ukate maana hata nchi unahiaribu. Unaona alichosema, ukikosa matunda haufai kwa chochote ila kukatwa na kutupwa motoni.

Kubali kulipa gharama…

Usife kibudu, kufa kibudu ni mnyama aliekufa Kabla ya kuchinjwa, huwa hafai kwa kuliwa, siunajua kibudu haliwi. Usikubali changamoto zikukatishe tamaa, usikubali kuishia njiani, usikubali usingizi na uvivu vikuue. Inuka tena pambana mpaka vitu vitokee. Ili baada ya kufa kwako Uendelee kuishi kwenye mioyo na akili za watu hapa Duniani. 

Usife kibudu, Pambana acha alama vizazi na vizazi vikufurahie.

Kufa kibudu ni ile hali ya kuondoka hapa duniani (kufariki) bila kuweka jitihada zozote katika kukamilisha au kufanikisha ndoto zako. Kwa maana ingine ni kuondoka na utajiri mkubwa ambao Mungu aliuweka ndani kwa visingizio mbalimbali, labda kwa kuogopa, Kujionea huruma, kushindwa kujinidhaminisha kwenye mambo ya msingi, kukataa maonyo na mengine mengi.

Ng’ombe akifa kabla ya kuchinjiwa tunamwita nyamafu hana faida tena hafai kuliwa, lakini akiwa amechinjwa tunaita nyama. Hii tunaifurahia na kuitumia kama kitoweo. Usiruhusu changamoto au maneno ya watu yaue ndoto zako, hakikisha unapambana kuona zikitimia.

Hivyo usife kibudu hakikisha unapambana kukamilisha ndoto zako ili baada ya kufa uendelee kuishi ndani ya mioyo ya watu.

FANYA HAYA.

Kwanza kabisa Mfanye MUNGU kuwa wa kwanza kwenye maisha yako, kwa kumpa muda wa kuomba, kusoma neno na kulitafakari. Mkabidhi Bwana Njia Zako nae atayanyoosha mapito yako.

1. Weka nidhamu binafsi kwenye mambo yote ya msingi unayopaswa kufanya, Jiwekee mipaka ya nini utafanya na nini hutafanya hatakama watu wote watakuwa kinyume na wewe. Kumbuka mipaka hii iwe inakusaidia kufikia ndoto zako na si kuwafurahisha wengi.

2. Andika tabia zote za kuacha ambazo zitakuzuia au kukuchelewesha kufikia ndoto zako. Dhamiria kuziacha na uanze kuchukua hatua.

3. Andika tabia za kujenga na kuimarisha ambazo zitakuwa sababu ya wewe kufikia ndoto zako. Alafu Chukua hatua.

4. Amua marafiki wa kuambatana nao ambao watakuwa sababu ya wewe kufika kule unapoenda. Kumbuka hufanyi kwaajili ya kumfurahisha mtu, bali ili kuhakikisha ndoto zako zinatimia. Watafurahia baadae wakiona matunda hatakama kwasasa hawakuelewi, songa mbele tu.

5. Hakikisha kila siku unaratiba yako ya siku. Hakikisha siku haipiti haujajiongezea thamani, kwa kuendelea kufanya vitu vya msingi tu. Na kuzikataa au kuacha mambo yanayokupotezea mda na tabia zisizokujenga. Kumbuka haukai milele hapa dunaini. Na una siku moja moja ya kuishi na sio mwaka mzima maana mwaka mzima ni mjumuisho wa siku mojamoja ulizoishi kwa siku mia tatu sitini na sita.


Nikukumbushe hiki. “Bad thought have to be rejected or chased away to leave and Good thought have to be assisted to stay.Mawazo mabaya (Tabia mbaya) hayawezi kuondoka mpaka uikemee, kuikataa  na kuifukuza LAKINI Pia Mawazo Mema (Tabia Njema) inahitaji msaada wako ili idumu. Jitihada zako ndo zitaamua.


Ghafla nikashtuka na kurevuka Kumbe ni mawazo tu. Maswali na mawazo mengi yazidi kurindima ndani ya kichwa changu.

Kazi kubwa aliyoniachia kutafakari na kutendea kazi.

Umeberikiwa sana.

Itaendelea ………….







HITIMISHO:

Maisha bila MUNGU ni sawa na chai bila sukari, inaweza kuwa na viungo vyote, ikanukia na kuvutia kila apitae maeneo hayo. Lakini ukiipeleka mdomoni hakika utatema, maana haiwezi kuwa na ladha . Ndivyo ilivyo maisha hayana ladha bila YESU, kwanje yanweza kuvutia kwa utajiri, mali na vitu ambavyo mtu anavyo ukijumlisha tabasamu fake analilitoa kuficha makovu na maumivu ndani ya moyo. Rafiki angu hapa siongelei dini maana mtu anweza akawa na Dini lakini asiwe na YESU, Sio wote wanaoingia shuleni ni wanafunzi.  

Hivyo kama huna YESU muda ni sasa, Mwamini kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yako. Kwa msaada Zaidi tupigie au tafuta kanisa la kiroho lililokaribu nawe. 



Itaendelea………….


Pata Makala mbalimbali ambazo zinapatikana kwenye website yake, Ya 

EMAGK SITE. 

Url: emaisra.blogspot.com 

Utazipata kwenye section ya INSPIRATION QUOTES au kwa kutumia search button kwa kuandika jina la Makala unalohitaji.

Baadhi ya Makala hizo.

1. Unachokitafuta sicho ulichokipoteza

2. Usiyoyajua kuhusu mavazi.

3. Mind pollution.

4. Mambo ya kuzingatia wakati unachagua kozi ya kusoma.

5. Mambo ya muhimu ya kuzingatia wakati unakumbuka sikuku yako ya kuzaliwa.

6. Nguvu ya mchakato.




SHUKRANI:

Kipekee nimshukuru MUNGU kwa kuniwezesha kuanda Makala hizi, Ni Neema ya pekee mno ambayo MUNGU amenipa na kuniwezesha kufanya kitu hichi kwa utukufu wake.

Pia nikushukuru wewe uliechukua muda wako kusoma na kujifunza mambo kadhaa kutoka kwenye Makala hii.








IMEANDALIWA NA 

EMANUEL ISRAEL KANGALA

0742 859 313

Website: EMAGK SITE.

Url: Emaisra.blogspot.com

22April 2022.

No comments:

Post a Comment