NAMNA YA KUITUMIA JANA YAKO LEO ILI KUJENGA KESHO YENYE UTUKUFU. - EMAGK SITE

Latest

This website was designed to help college student especially those who takes engineering course for review, past paper and other learning material. And teacher for review.

Friday, May 13, 2022

NAMNA YA KUITUMIA JANA YAKO LEO ILI KUJENGA KESHO YENYE UTUKUFU.

 

 

 SEHEMU YA KWANZA "1"

 

UTANGULIZI

Tunafahamu vyema kuwa panga hutumika kukatia kuni na kufanyia kazi zingine za nyumbani. Alietengeneza Panga alikusudia litumike kwa namna hiyo. Lakini panga linaweza kutumika kuondoa uhai wa mtu ambae ni kinyume kabisa na kusudi la mtengenezaji. 

Kumbe Kitu kinaweza kutengezwa kwa kukusudia kusaidia lakini anaekitumia akakitumia kwa kuumiza wengine au kujiumiza mwenyewe. Gari  ni zuri na alietengeneza alilitengeneza kwa kusudi zuri lakini likitumiwa bila kufuata utaratibu linaweza kusababisha kifo au maumivu makubwa kwa mtumiaji.

Ndivyo ilivyo ndugu yangu Mungu aliyagawanya majira na nyakati na kutupa uwezo wa kuikumbuka jana au majira na nyakati zilizopita, naam hata uwezo wa kuhifadhi hayo matukio kwa vizazi vingine ili tuitumie leo yetu vyema kwa kujifunza kutoka kwa waliotutangulia au matukio ya Jana. Maumivu au mafanikio yetu ya Jana yanapaswa kuwa sababu  ya kufanikiwa kwetu leo na sio sababu ya kufeli kwetu. 

Kwa kutokujua namna ya kutumia matukio na kumbukumbu zilizopita ndio sababu ya maumivu mengi tunayoyaona na Wengine tumeshindwa kupiga hatua kwaajili ya Jana Yetu. Badala ya Jana kuwa sababu ya kufanikiwa leo imekuwa sababu ya kushindwa kwetu.

"Matumizi mazuri ya Jana (kumbukumbu na matukio yaliyopita) yako yatakupeleka kwenye utoshelevu na matumizi mabaya ya Jana (kumbukumbu) yako yatakupeleka kwenye uhitaji, kufeli na kukata tamaa. Amuua kuitumia vyema Jana yako Leo kwa manufaa ya Kesho yako."

Tunayoyakumbuka leo ni mambo ya Jana, tulioyafanya, tuliyofanyiwa, tuliyoyasikia na tuliyoyasema, tuliyoyaona na tulioyaonyesha, tuliyotendewa na tuliyoyatenda. Kumbukumbu ya mambo haya yanaweza kukufanya ufanye maamuzi yatakayoijenga au kuibomoa kesho yako. 

Unakumbukumbu gani? Unachokikumbuka unakitumiaje kwaajili ya kuijenga kesho yako?

Kwenye maandiko matakatifu kuna mahali Mungu anasema "Usiyakumbuke mambo ya zamani......" Hapa alikuwa anamaanisha nini?  Je nauweza nikasahau maumivu niliyopitia jana?

Mafanikio yangu ya JAna yanaweza kuwa kikwazo kwa mafanikio yangu ya kesho?

Kufeli kwangu au kushindwa kwangu Jana inaweza kuwa sababu ya kushindwa kwangu leo? Historia na kumbukumbu ya Jana inweza ikaathiri vipi Leo yangu na Kesho yangu? kivipi? (Usikose sehemu ya pili ambapo tutayaangalia maswali haya muhimu ili kujua namna ya kutumia Jana yangu ili kujenga kesho yenye utukufu.)

Tuangalie sehemu hii ya kwanza ya namna ya kuitumia Jana yako kama Mungu alivyoikusudia ilikuijenga kesho yako.

SEHEMU YA KWANZA (utangulizi)


JANA itufundishe namna ya kuishi leo, ili kesho yetu iwe yenye utukufu.


Jana au matukio yaliyopita kwenye maisha yetu, yawe mazuri au mabaya, yanapaswa yatufundishe namna ya kuishi leo ili kuifikilia kesho yenye utukufu. Hivyo kila unapoangalia nyuma, utakayoyaona yakufundishe namna ya kuishi leo, yakutie moyo kuendelea mbele Zaidi, ya kupe ujasiri wa kupambana Zaidi, Mengine yakufanye uongeze juhudi kwa kuichukia hali ile ya mwanzo na kutaka kuwa bora Zaidi ya Jana yako.

Kuna mambo tunapaswa kuyakumbuka ili yatupe nguvu ya kukabili changamoto tunayokumbana nayo sasa.

Usiwaogope, kumbuka sana Bwana Mungu wako, alivyomfanya Farao na Misri yote. (Kumbukumbu 7:18)

Embu kumbuka namna MUNGU alivyokusaidia na kukupitisha kwenye changamoto ulizopitia, Namna alivyopigana na adui zako na kulidhibitisha Neno lake Juu yako. Hata sasa usiogope changamoto unayoipitia bila kujali ukubwa wake, KUMBUKA yale MUNGU aliyokutendea tangu ukiwa mtoto hata sasa, alivyokutetea shuleni, chuoni, kazini na kwenye maisha yako kwa ujumla. Hata sasa atakutetea tena. Usiogope Endelea mbele, usiache hiyo Biashara kwasababu ya hiyo changamoto, usiache huduma kwasababu ya changamoto hiyo. Endelea mbele PANGA VITA UPYA Mungu yuko upande wako.

 

 

(Usitishwe na ukubwa wa Goliatia kumbuka Mungu alivyowatia DUBU na simba mikononi mwako, Hata huyu mfilisti atakuwa kama mmoja wao.)

Unachangamoto kwenye Huduma yako au Biashara?

Kumbuka aliekuruhusu uanze hawezi kukuacha uishie njiani, Songa mbele.

Je kila siku unaona kufeli kwenye biashara yako? Au Taasisi unayoiongoza?

Kumbuka wanawa Israeli walipigwa na ndugu zao Zaidi ya mara tatu, Baada ya MUNGU kuwaruhusu kupigana nao. Waamuzi 20:1-48, 21..(stori nzima iko hapa)

Usihofu, usikate tamaa bali badili mbinu ya namna ya kufanya biashara unayoifanya, namna unavyotatua matatizo yanayoibuka katika taasisi, jitahidi kuwa muwazi kwa unaowaongoza. Tumia muda wa kutosha kufikiria juu ya taasisi na namna ya kuboresha kwa maslahi mapana ya Taasisi.

Jitahidi sana makosa uliyoyafanya jana yasijirudie leo, nayale mazuri ya jana uyaboreshe leo.

 (Basi kumbuka ni wapi ulikoanguka, ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza, lakini usipofanya hivyo, naja kwako, name nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.  ufunuo2:5).

Badilika fanya tofauti na ulivyofanya jana.

Unataka kuoa au kuolewa na unahisi muda umeenda sana na bado huelewi?

Kumbuka Kisima kipo mbele yako upo karibu sana na kijito cha Maji kama Hagai, Macho yako yakafumbuliwe, Ukaone vyema.

Je Familia imekutenga na kukuchukia bila Sababu?

Mkumbuke Yusufu pamoja na kutengwa na familia yake haikuwa sababu ya yeye kuizika ndoto yake. Kumbuka MUNGU anakupenda usijichukie hata wote wakikuchukia, Kaza mwendo kuikabili hali yako ili jina la Bwana litukuzwe kama lilivyotukuzwa kupitia YUSUFU.

JE kazini wamekusingizia? Umefukuzwa kazi Bila sababu?

Kumbuka Yusufu alifukuzwa kwenye nyumba ya Potifa na kutiwa gerezani, na Hiyo ndiyo iliyokuwa hatua yakuelekea IKULU na kuiongoza nchi nzima ya MISRI. Inawezekana kufukuzwa kwako kwa kuonewa ndio sababu ambayo MUNGU anaitumia ili kukuinua Zaidi. 

#inuka tena Acha kulia

#Fanya kiume.

 

Tujifunze kwenye historia yetu naya wliotutangulia na sio kudumu kwenye maumivu ya Jana.

#Wewe ni wa thamani sana hii ndio sababu, bila kujali makosa na dhambi ulizokuwanazo  YESU  alikuja na kufa msalabani kwaajili yako.

 

TIPS:

1.     1. Hauruusiwi kukata tamaa kwenye kuuendea ukuu wako, Bila kujali ukubwa wa changamoto unayokutana nayo.

2.      2. Ukifeli kwenye kitu au biashara unayofanya haimaanishi kwamba wewe ni kilaza Bali inamaana badili njia ya kufanya.

3.      3. Kumbuka hauruhusiwi kufanya kila kitu kwasababu wengine wanafanya, Bali kuna wakati utapaswa kujinyima ili kuifikilia ile thawabu iliyo mbele yako.  1cor 9:25

4.      4. Kuna kumbukumbu zingine zinaumiza ila unapaswa kuzikumbuka ili zikupe nguvu ya kuendelea mbele, nguvu ya kuongeza mwendo Zaidi. Na ujasiri wa kutokukata tamaa wala kutamani maisha ya jana. Hasa kukumbuka namna ulivyotoka au namna ya kutoka na namna unavyotakiwa kuishi iliusirudi kwenye maumivu ya jana.

  Kumbukumbu 16:12 “..Nawe kumbuka kwamba ulikuwa mtumwa huko misri, tena zishike amri hizi kwa kuzifanya” Kumbukumbu 24:18, 22

5.      5. Kuna wakati unapaswa kukumbuka namna ulivyoanza, ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia ilikujua wapi ulikosea au unapopaswa kuongeza juhudi au kuboresha Zaidi ili kuijenga kesho yenye utukufu. ( “Basi kumbuka jinsi ulivyopokea na jinsi ulivyosikia, yashike hayo na kutubu …..” Ufunuo3:3

“Basi kumbuka ni wapi ulikoanguka ukatubu ukafanye matendo ya kwanza….” Ufunuo 2:5

 

INAENDELEA,

USIKOSE

SEHEMU YA PILI.



IMEANDALIWA NA

EMANUEL ISRAEL KANGALA

0742 859 313

Website: EMAGK SITE.

Url: Emaisra.blogspot.com

13MAY 2022.

 


No comments:

Post a Comment