Chochote ambacho MUNGU ameweka kwako sio chako ni kwaajili ya watu na
jamii inayokuzunguka, Sio kwafaida yako ni kwa faida ya wengine, Hii hamaanishi
kwamba wewe ni wa muhimu sana kushinda wao, la hasha bali umeaminiwa kupewa
ulichopewa kuwa utakifikisha kwa watu waliokusudiwa kwa namna sahihi, muda
sahihi, ilimfae kila mmoja aliekusudiwa.
Kila mmoja ni wa muhimu, do you
know why? Kila mmoja amebeba kitu cha pekee kwaajili ya faida ya wengine.
Ukiidharau cha mwenzako umedharau na kuicheka kesho yako. Maana sio kwaajili
yake amepewa kwaajili ya mapungufu uliyonayo.
1korintho 12:4 BASI PANA
TOFAUTI YA KARAMA, BALI ROHO NI YEYE YULE, TENA PANA TOFAUTI YA HUDUMA BALI
BWANA NI YEYE YULE. TENA PANATOFAUTI YA KUTENDA KAZI BALI MUNGU NI YEYE
YULE AZITENDAYE KAZI ZOTE KATIKA WOTE. LAKINI KILA MMOJA HUPEWA UFUNUO WA
ROHO KWA KUFAIDIANA. MAANA MTU MMOJA KWA ROHO HUPEWA NENO LA HEKIMA NA
MWINGINE NENO MAARIFA BALI ROHO NI YEYE YULE …….
Karama aliyenayo mwenzako ndiyo
uhitaji wako, HUduma alie nayo mwenzako ndio unayohitaji ilikupiga hatua,
lakini pia mnaweza makafanana huduma lakini utendaji kazi ukatofautiana jua
hivi ulipewa kwaajili ya wengine. Utofauti wa utendaji kazi wa huduma ni
kwaajili ya kusaidiana na kuhudumiana kwa wenye huduma inayifanana naam na
wenye huduma zingine pia. Niruhusu nitumie mfano wa kipaji cha michezo kuelezea
zana hii. Kwenye mchezo wa mpira wa miguu, kuna makundi matatu (unaweza
kuyagawanya Zaidi ya hapo) kundi la kwanza ni wachezaji, wawezeshaji na la
mwisho mashabiki au wanufaikaji wa mchezo. Maana namna aliyepewa inawezekana
isimfaidie yeye bali waliomzunguka. Kumbuka kazi ya karama ni kufaidiana na sio
kumnufaisha mwenye karama au kipaji. ( kuna marupurupu na Lengo, kuwa makini)
Hahahaha mkono hauwezi
kujishika mwenyewe utashikwa na mkono mwingine, Tunahitajiana sana.
1korintho12:12
Ukiona unajimwamba fai kama
asemavyo rafiki wa seremala, pstr Raphael lyela, ujue kabisa ndio mwanzo wa
kunyauka kwako, na sifa pekee itakayokubeba na itakayobebwa ni ya Jana yako
huku leo yako ikijaribu kufuta kwa bidiii sifa njema uliyoitengeneza jana, kwa
karama na kipaji alichokupa MUNGU.
Mkono unahitaji kusafishwa na mkono mwingine, huwezi
kujisafisha mwenyewe, Ndivyo ilivyo mwalimu anamwihitaji mwalimu iliawe bora
Zaidi na kufaa mbele za MUNGU, Nabii anamuhitaji pia Nabii mwingine iliakue na
kuongezeka katika kimo akimpendeza MUNGU na wanadamu, kama jicho
linavyomuhitaji mtu mwingine kumtazama na ilikuona kama kuna kuna uchafu au
mdudu ili mikono ifanye kazi yake vyema.
No comments:
Post a Comment