VIGEZO AMBAVYO HUPASWI KUTUKIA WAKATI WA UCHAGUZI WA FANI/KOZI YA KUSOMA. - EMAGK SITE

Latest

This website was designed to help college student especially those who takes engineering course for review, past paper and other learning material. And teacher for review.

VIGEZO AMBAVYO HUPASWI KUTUKIA WAKATI WA UCHAGUZI WA FANI/KOZI YA KUSOMA.

 


uchaguzi wa nini ukasome au kozi gani usomee ni kati ya maamuzi ya maana na ya kuzigatia sana, maana huathiri maisha yako kwa ujumla baada na wakati unasoma.

Lengo mama la kusoma ni ili mtu apate ujuzi utakaomsaidia kuleta mabadiliko chanya na kutatua matatizo yanayoikumba jamii husika, ili kuleta maendeleo kwa jamii na kwake binafsi.

Kuna kauli hii "SOMA ULE" tumekuwa tukiambiwa na kuisikia kutoka kwa wazazi, ndugu, marafiki na jamii inayotuzunguka. Niseme wazi kwamba kauli hii haifai na imechochea watu wengi kufikiria kusoma kozi ambayo ataweza kufanya ujanja ujanja ili afanikiwe haraka kiuchumi bila kujali maumivu atakayoacha kwa jamii au kampuni husika.  Mtazamo huu umeua ujuzi na ubunifu kwa wahitimu wa kozi mbalimbali na kuzalisha wasomi wengi ambao wanarudi mtaani kusaka Ajira, na Ajira zenyewe hazionekani. 

MIMI NASEMA UKIWA UNAENDA KUSOMA NENDA NA KAULI HII "SOMA UPATE MAARIFA"  Ibaki kazi kwako kuyabadilisha maarifa hayo na kuwa fursa itakayokuingizia kipato.

Kuna makosa ambayo nilifanya au wengi tulifanya na sitamani uyarudie.

ifuatayo ni vigezo ambavyo hupaswi kuvitumia wakati unafanya uchaguzi wa kozi/fani ya kusoma.

yafuatayo ni baadhi ya vigezo ambavyo hupaswi kuvitumia kama vigezo mama wakati unachagua kozi ya kusoma.

A)     KIGEZO CHA AJIRA MTAANI AU MSHAHARA MREFU:- kigezo hiki watu wengi na wanafunzi hupenda kukitumia wakati wa uchaguzi wa fani au kozi ya kusoma.
VITU VYA KUFAHAMU HAPA:
Swala la ajira lina yumba yaani halikoimara miaka yote. Kozi ambayo unahisi haina ajira kwa haraka kwa sasa, miaka michache iliyopita kozi hiyo ilikuwa lulu mtaani.

Nikukumbushe kidogo, miaka michache iliyopita kozi ya ualimu ilikuwa ni kozi ambayo ukimaliza kusoma unapangiwa ajira moja kwa moja na serekali, lakini sivyo ilivyo sasa, walimu wamejaa.

Point yangu ni hii, unaweza ukaanza kusoma hiyo kozi na ndani ya miaka yako mitatu ya kusoma, huku mtaani pakawa tayari pa mejaa, na ukitoka utaanza kusota mtaani kwasababu huwezi kutumia ujuzi wako kwa ufasaha na furaha kwasababu kilichokufanya kusomea kozi hiyo ni upatikanaji wa ajira. Hivyo utakuwa muhanga wa kuililia serekali kwa ukosefu wa ajira huku uliosoma nao wakiendelea kunufaika na maarifa waliyopata.

Namba 2: unaweza ukapata hiyo kazi kweli lakini ukafanya kwa viwango vya chini na ikawa kama mzigo mkubwa kwako kwamaana kilichokufany usomee kazi hiyo ni ajira na Pesa.

Chukulia mfano wa manesi na watu wengine wa sekta ya afya, utaona tu dhahiri aliesomea ili apate ajira na pesa kwenye namna wanvyowachukulia na kuwahudumia wagonjwa, mwingine haoni shida mgonjwa akifia hospitalini mbele yake kwasababu ameshindwa kumpa kitu kidogo, kwa kifupi hajali wagonjwa.

Hata walimu wasiokuwa na wito wa ualimu huwa wanonekana kwenye namna ya ufundishaji wake, kunamwingine hajali mwanafunzi kuwa atafaulu au la, kunawengine wanajitahidi wafaulishe ili wasifukuzwe kazi lakini huwa ni mzigo mkubwa sana ambao wanatamani ifike siku wautue mzigo huo.(AJIRA, PESA, MAFANIKIO HIVI VITU NI VIZURI SANA LAKINI JITAHIDI SANA USIWE MTUMWA WA HIVYO MAANA VITANYANG’ANYA FURAHA YAKO NA AMANI YA MOYO WAKO.)
 ONYO: USISOME KOZI KWASABABU INAAJIRA AU MSHAHARA MREFU MTAANI. UTAUMIA.

B)     KUSOMA KOZI KWASABABU MZAZI AMEKUAMBIA. KOZI AMBAYO HAUIFURAHI NA HAIKUPI MWELEKEO MBELE BASI HAINA HAJA YA KUPOTEZA MUDA KUISOMA ACHANA NAYO. KUNA WATU WENGI AMBAO WALICHOSOMEA KWASABABU YA MSUKUMO WA WAZAZI AU PESA AU AJIRA, WALIACHA NA KUANZA KUFANYA WALICHOKIPENDA.

"WATU WALIOFANIKIWA HUFANIKIWA KWA KUFANYA VITU WALIVYPENDA NA SI VITU WALIVYOLAZIMISHWA KUSOMEA KWA VIGEZO VYA AJIRA NA MSHAHARA MNONO AU RAFARIIIZIII WAJULIKANAO SASA.”

EPUKA KUPOTEZA MUDA KAMA KWELI UNATAKA UFANIKIWE SOMA KOZI UNAYOIPENDA AMBAYO UKO TAYARI KUIFANYA HATA KWA MSHAHARA KIDOGO NA UKAIFURAHIA
          
          Je unaona Nini kwenye kozi yako unayotaka kusoma nje na ajira?




......BY:
..........   Emanuel Israel KANGALA.
0742859313
       emanuelkangala@gmail.com


No comments:

Post a Comment