New
hahhaha,
ilikuwa nzuri sana kuwatazama wawili hawa namna walivyopendana utasema mapacha kumbe ni mtu na baba yake naam alikuwa ni muumba wake pia,
kijakazi mmoja katika jumbe lile la kifalme alichukia sana kuona mahusiano yale yakizidi kushamiri, akaamua kujifanya rafiki kwa mtoto mwisho alifanikiwa kuiaribu mahusiano yale, mtoto alibadilika na kuacha kumtii baba yake.
BABA Yake aliamua kumfukuza na kumuondoa mwanae ktk jumbe lile la kifalme huku akiwa na mipango mizuri kwa mwanae.
upande mwingine mtoto huyu aliendelea kumsahau kabisa baba yake huku akitumikia na kuyumbishwa na dunia,
uzao wa mtoto huyu uliendelea kutoka familia hadi vizazi na vizazi, kila kizazi kilibadili imani kutoka imani moja kwenda nyingine kwani hawakuifahamu asili na imani halisi ya baba yao.
muda, ulifika BABA ambae ni muumbaji wa mtoto huyu alimkumbuka mtoto wake na kizazi chake, hakika aliuzunika sana alipoona uzao wa mwanao ukiyumbishwa na kuteswa na adui yake. akakumbuka ahadi zake nyingi alizoweka na watumishi wake, hakika hakusita kuwarudisha wanawe katika ufalme wake.
iliniuzunisha sana pale nilpoona wengi wakikataa kurudi katika ufalme wa BABA yao na katika imani halisi ya BABA yao kwani furaha ya kweli haipatikani popote pale nje na nyumbani. kwani kuna wengi waliongopa kurudi kwenye ufalme wao kwa kutokujua kwani wengine walisema hii ni dini ya baba yangu mimi siwezi kuiacha, na kauli hii ilidhirisha kuwa waliogopa vitisho walivyovikuta kuwa ukiacha njia hakika utalaaniwa na hatutakuwa na ushirika na yeyote alieacha njia hii.
BABA yule alifanikiwa kuwarudisha wachache katika ufalme lakini aliendelea kuwasisitiza kila leo ili warudi kwenye ufalme wao na wafaidi matunda ya baba yao.
TAFAKARI
adamu alimuasi MUNGU na kuangukia katika laana
watoto wake pia waliendelea katika uasi huo
mababu zetu pia waliaabudu Miti, mawe na mizimu wakiendelea katika uasi.
sasa hivi hakuna anae abudu miti au mawe hivyo ukisema utaki kuasi dini ya baba yako hakika haufahamu unachokisema kwani hata baba yako aliasi dini ya baba yake akitafuta amani ya moyo naam na zaidi kuliko amani. Hata babu yako hivyo hivyo naye aliasi dini ya baba yake, naam na adamu na yeye aliasi, HIVYO USIOGOPE KUUFUATA UKWELI KWA KUOGOPA KUASI DINI YA BABA, LAANA NA MENGINEYO, kwani baada tu ya admu kuasi tulianza kutembea chini ya laana, ILA YUKO ALIEKUJA KUTURUDISHA NYUMBANI NA KUIVUNJA ILE LAANA SI MWINGINE NI YESU KRISTO,
HAKUNA LAANA ITAKAYOKUPATA UTAKAPORUDI NYUMBANI.
BABA ANAKUSUBIRI
FANYA UAMUZI SASA WA KUMPOKEA YESU KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO, HAUTAJUTA MAISHA YAKO YOTE...
TULIO KWA YESU TUNEFURAHIA NEEMA YAKE.. (UNAWEZA UKAWA KWENYE DINI USIWE NA YESU, BADO HUJACHELEWA FANYA MAAMUZI)
MWAMINI LEO
RUDI NYUMBANI
By:-
emenuel israel.
0742859313
Facebook:
emmanuelisrielity@gmail.com
No comments:
Post a Comment