USIYOYAJUA KUHUSU MAVAZI - EMAGK SITE

Latest

This website was designed to help college student especially those who takes engineering course for review, past paper and other learning material. And teacher for review.

USIYOYAJUA KUHUSU MAVAZI



Contents

1. UTANGULIZI 2

2. SEHEMU YA KWANZA. 3

Je wajua mavazi ya kwanza yalitengezwa na nini? Je wajua mbunifu wa kwanza wa mavazi ni nani na alitoka nchi gani?. 3

3. SEHEMU YA PILI 4

BIBLIA INAZUNGUMZIAJE UVAAJI WA MAVAZI?. 4

SASA JE BIBLIA INAONGELEAJE UVAAJI WA MAVAZI YASIYOSTIRI MIILI NA YASIYO NA ADABU?. 4

4. SEHEMU YA TATU.. 5

JE NI KWELI KWAMBA MAVAZI NI UTAMBULISHO? YANAKUTAMBULISHAJE?. 5

JE JAMII  INAONGELEAJE  UVAAJI  WA  MAVAZI?. 6

5. SEHEMU YA NNE. 7

SEREKALI INASEMA NINI KUHUSU MAVAZI?. 7

6. HITIMISHO.. 13

 

 

UTANGULIZI
Je wajua mavazi ya kwanza yalitengezwa na nini?
Je wajua mbunifu wa kwanza wa mavazi ni nani na alitoka nchi gani?


πŸ‘‰ Kuna mkanganyiko mkubwa sana kuhusiana na mavazi unaondelea katika jamii, baina ya wazazi na watoto, na kwenye nyumba za ibaada pia, wengine wakisema ni ruksa kuvaa utakavyo huku wengine wakipinga hilo. Naamini kabisa kuwa ili kitu kitumike ipasavyo ni lazima turudi kwa yule aliekitengeneza, tujue kwanini alitangeneza? na alitengeneza ili kitumikaje? Ni ukweli usiopingika kwamba kitu kinaweza kuboreshwa bila kuondoa maana ya mtenganezaji. Makala hii inaweza kukusaidia na kukupa mwanga ya USIYOYAJUA KUHUSU MAVAZI.

 


 


SEHEMU YA KWANZA


Je wajua mavazi ya kwanza yalitengezwa na nini?
Je wajua mbunifu wa kwanza wa mavazi ni nani na alitoka nchi gani?

kabla hatujaenda kwenye mavazi ya kwanza yalitengenezwa na nini, tuanze kwa kujua nini maana ya mavazi?
mavazi ni nguo au kitu kilichotengezwa na material mbalimbali yanayotumiwa na wanadamu ilikusitiri miili yao. Tunafahamu pia kuna aina nyingi sana za mavazi. Na mavazi haya hutengenezwa kwa material tofautitofauti. mfano. yako yale yanayotengenezwa na ngozi, pamba, katani n.k


sasa basi "Mavazi ya kwanza yalitengenezwa na nini? na nani aliye tengeneza mavazi hayo? na kwanini alitengeneza? Na kunaumuhimu gani wa mavazi katika kipindi hiki cha sasa.? Kuna aina ngapi za mavazi hadi sasa?" karibu tuendelee kudadafua TUSIYOYAJUA KUHUSU MAVAZI.


Majibu ya maswali haya yanaweza kutusaidia kuondoa mkanganyiko ulioko katika jamii kuhusu mavazi naaam hata katika nyumba za ibaada.


πŸ‘‰ mavazi ya kwanza kutengenezwa yalitengenezwa kwa ngozi za wanyama. Mavazi haya yalitengenezwa kwa ustadi wake.... Kwamara ya kwanza kabisa yalitengenezwa na MUNGU mwenyewe.. Na kuvaliwa kwa Mara ya kwanza na adamu na hawa..

 Mwanzo:3.21
Bwana Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.


Sasa tukiangalia hapa, Dunia nzima kulikuwa na watu wawili tu, sasa Je kwanini Mungu aliwatengenezea mavazi ya ngozi? ukizingatia mwanzo wao wenyewe walijifunika kwa majani. Lakini Mungu akaona haitoshi akaaamua kuwatengenezea mavazi ya ngozi.
Lengo kuu la mtangenezaji lipo wazi kabisa ambalo ni kusitiri miili ya watu. Hapa tunaona kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kusitiri Mwili kulingana na namna alivyotuumba. Je kama Mungu aliona umuhimu wa mavazi kwa watu wawili Je si zaidi sana kwasasa kwa mabilioni ya watu?

 

 

 

 

 

 

 

 

 

SEHEMU YA PILI

BIBLIA INAZUNGUMZIAJE UVAAJI WA MAVAZI?

Biblia inasisitiza watu kujipamba kwa mavazi yanayositiri pamoja na Adabu nzuri.

1timotheo 2:9-10 ;vivyo Hivyo WANAWAKE Na Wajipambe Kwa Mavazi YA KUJISITIRI Pamoja na ADABU nzuri,....; NB.
Pigia Mstari KUJISITIRI NA ADABU NZURI,

Kumbe mavazi yanaweza kuwa ya kujisitiri lakini yasiwe na adabu nzuri. (watch out?) Mavazi yanayofaa katika jamii ni yale yanayositiri miili pamoja na adabu nzuri.

Note: Kumbe nguo inaweza kufika mpaka chini lakini isiwe na adabu nzuri. Hapa swala si kuvaa tu mavazi ya kujisitiri Bali ni Muhimu pia yawe na adabu nzuri.

SASA JE BIBLIA INAONGELEAJE UVAAJI WA MAVAZI YASIYOSTIRI MIILI NA YASIYO NA ADABU?

Katika Jamii kuna mavazi yajulikanayo kama mavazi ya kikahaba, haya ndiyo yale yasiositiri miili vizuri na yasiyo ya adabu. Na kwa asilimilia kubwa mavazi hayo hutengenezwa kwa lengo la kuamsha tama ya mwili.

 

Mithali:7.10
Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo;

NOTE: “Biblia inatambua uwepo wa mavazi ya kikahaba”

MUNGU ANATANBUA MWILI WAKO KAMA HEKALU LAKE HIVYO ATAKAE LIHARIBU NA YEYE ATAMUHARIBU.

ANAUTHAMINI MWILI WAKO ANATAMANI UTHAMINI PIA, UVIKE VIZURI SAWASAWA NA MATAKWA YAKE NA KUUTUNZA NA KUWA KIELELEZO KATIKA MAVAZI NA MWENENDO.

 

JE MUNGU ANAANGALIAJE UVAAAJI WA MAVAZI? JE NI HALALI KWA MTU KUVAA MAVAZI YOYOTE YALE MBELE ZA MUNGU? MAVAZI YANAATHIRI VIPI UHUSIANO WAKO NA MUNGU? MAVAZI YANAUWEZO WA KUKOSESHA MBINGU?

Tuendelea kuangazia tusiyoyajua kuhusu MAVAZI. Tuendelee kujifunza pamoja.

1samweli

“Siangalii kama wanadamu waangaliavyo, wanadamu wanaangali mwili ila mimi natazama ROHO.”

Hapa Mungu alikuwa anamwambia samweli kuwa YEYE haangalii kama Binadamu waangaliavyo maana Sisi tunaangalia kwa nje tu na hatuwezi kuona ndani ya mtu (Roho yake).  Lakini yeye hutazama vyote yaani mwili na Roho. Na hi indo sababu Mwili ni hekelu lake.

Jiulize pia, MUNGU kama anaangalia ROHO tu Je kwanini alitengeneza mavazi ya ngozi kwa adamu na Hawa? Na kipindi hicho walikuwa wawili tu, Je si zaidi sana kwa mabilioni ya watu sasaivi?

 

 

SEHEMU YA TATU

 

JE NI KWELI KWAMBA MAVAZI NI UTAMBULISHO? YANAKUTAMBULISHAJE?

Mavazi yanaweza kutambulisha kazi yako.

 



Mavazi pia yanaweza kutambulisha eneo au mandhari uliyopo kwa wakati huo. Kuna mavazi yanayovaliwa maeneo maalumu tu. Kama mavazi ya michezo, kuogelea n.k





 HUWEZI KWENDA KWENYE RIDHAA NA SUTI MY FRIEND UTAKUWA KITUKO KAMA ILIVYO PIA HUWEZI KWENDA NA NGUO ZA RIDHAA KANISANI AU KUPIGA NAZO MISELE.

“KILA VAZI NI ZURI KWENYE ENEO LAKE”

Mavazi yanaweza kuakisi tabia yako. Ni kweli kwamba unaweza vaa mavazi yanayotambulisha tabia Fulani ambayo kiuhalisia wewe hauna ila uliona tu mtu Fulani amevaa na wewe ukapenda kuvaa Bila kutafuta sababu. Tunza muonekano wako.


JE JAMII  INAONGELEAJE  UVAAJI  WA  MAVAZI?

Katika kila Jamii Duniani inatambua uwepo wa mavazi mbalimbali. Katika Jamii zetu za kiafrika inatambua kuwa kuna mavazi ya kulalia, kuogea, kuogelea au Ufukweni, na pia uwepo wa mavazi ya kikahaba.

 

NB: Ukivaa mavazi bila kuzingatia eneo unaweza kuwa kituko mbele ya Jamii. Kila mavazi yanaumuhimu wake katika eneo husika tu, na hupoteza maana nje ya Eneo.

Kwamfano: Huwezi vaa mavazi ya kulalia wewe ukapiga nayo misele au kwenda nayo kanisani. Hakika utaonekana mwehu.

Huwezi vaa mavazi ya michezo na kwendanayo ofisini.

Utaonekana Mwehu kwasababu umevaa mavazi ambayo si sehemu yake husika.

Hivyo Uvaaji wa Mavazi uzingatie eneo, au Kazi unayoifanya.

 

MAVAZI YA KIKAHABA NI YAPI? JAMII INAYATAMBUA?

Haya ni mavazi yale yasiyositiri miili vizuri na yasiyo na adabu, Mavazi haya huamsha taamaa za mwili. Na lengo kubwa la utengenezwaji la mavazi haya ni kuwavutia wanaume kimapenzi. Zingatia hili uvaaji wa mavazi haya  kwa mabinti au wanawake hauwafanyi wanaume wawapende bali unawavutia kwa mapenzi tu.

Aina hizi za mavazi hupigwa marufuku katika jamii tunazoishi. Ingawaje kwa asilimia kubwa sasa Jamii imeanza kufifia katika upingaji wa uvaaaji wa mavazi haya kwa kile VIJANA wanachokiita kizazi cha kisasa na kuporomoka kwa maadili kwa kasi katika Jamii zetu.

“mavazi ya kulalia ukipiga nayo misele yanageuka na kuwa mavazi ya kikahaba maana yanaonyesha maungo ya mwili ambayo yanapaswa kusitiriwa katika kadamnasi ya watu”

Kila jamii inasheria na mipaka yake, mavazi yanaweza kuwa ya heshima katika eneo Fulani lakini yakaonekena ya ovyo katika eneo lingine.

SEHEMU YA NNE

SEREKALI INASEMA NINI KUHUSU MAVAZI?

Serekali inatambua uwepo wa aina mbalimbali z mavazi, Kwenye ofisi zote za serikali mavazi yanayokubalika kuvaliwa kwa njinsia zote ni yale ambayo yanasitiri miili vizuri na yana adabu nzuri, Kinyume na hapo hayaruhusiwi kabisa, imefika mahali hadi wateja au wanaohitaji huduma kulazimika kuvaa mavazi yanayositiri miili yao ili kuipata huduma hiyo.

MWANASHERIA MKUU AKIFAFANUA KUHUSU MAVAZI

“……………… Akifafanua Mwanasheria Mkuu alisema Sheria ya kudhibiti mavazi ipo namba 1 ya mwaka 1973 ambayo inaitwa sheria ya kulinda utamaduni wa Taifa.

Alisema sheria hiyo inafanya kazi na haijafutwa, ingawa alisema tatizo lake ni utekelezaji wa sheria hiyo na kwamba ndio maana wananchi wamekuwa wanakiuka kanuni za mavazi ikiwemo kuvaa nguo fupi zinazoonesha mwili wa binadamu ………….”

Kutoka (chanzo)

 https://habarileo.co.tz/habari/sheria-kudhibiti-mavazi-yasiyofaa-ipo.aspx

tarehe 12/12/2013


SHERIA ZA MAVAZI KWA WATUMISHI WA UMMA

 

SOURCE (CHANZO): https://www.tanzania.go.tz/egov_uploads/documents/WARAKA_WA_MAVAZI_Na_en_sw.pdf

 

 “WARAKA WA UTUMISHI WA UMMA NA 3 WA MWAKA 2007 KUHUSU MAVAZI KWA WATUMISHI WA UMMA



Kwa Wanawake

 (i) Baadhi ya mavazi yasiyofaa:

• Nguo zinazobana,

• Nguo fupi ambazo zinaacha magoti wazi.

• Nguo ambazo zinaacha sehemu ya mwili wazi kama vile kitovu na kifua,

 • Nguo ambazo zina picha, michoro, na maandishi ambayo hayaendani na shughuli za serikali,

• Kaptura aina yoyote ile kama vile pedo na pensi,

• Nguo zinazoonyesha maungo ya mwili (transparent).

• Suruali za “Jeans”,

• Suruali yoyote iliyoachwa bila kupindwa,

• Fulana – “T-Shirts” (Hizi zivaliwe tu wakati wa shughuli maalum inayotambulika),

3 • Nguo ambazo ni za kazi maalum – michezo, kazi za nje au burudani. Hizi zivaliwe mahususi wakati wa utekelezaji wa shughuli hizo,

 • Nguo yenye maandishi ya chama chochote cha siasa au ushabiki wa kitu fulani,

• Nguo yeyote inayopingana na maadili ya utumishi wa umma.”

 

Kwa Wanaume

(i)                Baadhi ya mavazi yasiyofaa:

• Nguo ambazo ni za kazi maalum kama vile michezo (Hizi zivaliwe wakati wa shughuli hiyo tu).

 • Nguo ambazo zina michoro, maandishi na picha ambazo haziendani na shughuli za serikali.

 • Nguo zinazobana,

• Kaptura ya aina yoyote.

• Suruali yoyote inayoachwa bila kupindwa.

• Suruali za “Jeans” na Fulana “T-shirts” (Hizi zivaliwe tu wakati wa shughuli maalum inayotambulika).

• Kikoi au msuli

• Nguo zenye maandishi ya chama chochote cha siasa na yenye kuonyesha ushabiki wa kitu fulani.

• Nguo yeyote inayopingana na maadili ya utumishi wa umma “

 

JIFUNZE KITU HAPO JUU:

NGUO AU MAVAZI YANAYOPIGWA VITA NI YALE YASIOSITIRI MIILI WALA KUWA NA ADABU NZURI.

 

 

HITIMISHO


πŸ‘‰ Biblia inatambua kuwa kuna mavazi ya kikahaba... Mithali:7.10 Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo;


πŸ‘‰ Serekali inatambua kuwa kuna mavazi ya ofisini, kazini na sehemu mbalimbali..
πŸ‘‰ jamii inatambua kuwa kuna mavazi kikahaba, ya kulalia, kazini n.k., jamii hukemea uvaaji wa mavazi yasiofaa,,, kama mavazi ya kikahaba....


πŸ‘‰kanisa limekaa kimya.......
Na wengi kusema kuwa MUNGU anaangalia roho... Hivyo hawana haja na mavazi unayovaa yaani hata ukiamua kwenda na chupi kanisani hawana shida cha msingi roho yako iwe safi mbele za MUNGU...Hii inaumiza sana watu wameshindwa kutambua uthamani wa wao kwake mwenyewe na kwa wengine....


πŸ‘‰ jiulize maswali haya kama MUNGU anaangalia roho... Je kulikuwa na haja gani kwa MUNGU kuwatengenezea mavazi adamu na hawa..? Kumbuka kipindi hicho dunia nzima walikuwa ni wako wawili tu... Kama MUNGU aliona umuhimu wa mavazi wakati walikuwa wawili tu,,,, je si Zaidi sana kwa sasa ambao tupo mabilioni ya watu? Kama MUNGU, serilikali na jamii inayatambua mavazi ya kikahaba, je wewe ni nani hadi upinge? Je hayo mavazi ya kikahaba waliyaonea rohoni?


πŸ‘‰ naongea na wewe.... Mavazi unayovaa unajua kabisa serekali imeyakataa, jamii imeyakataa hata ukijitia moyo kwamba MUNGU anaangalia roho, jua MUNGU hatakukubali na unahatari kubwa ya kuingia motoni ....
Hivi jiulize unaenda kanisani na mavazi ambayo hata serekali imeyakataa kuingia nayo katika ofisi zake,, jamii imezikataa... Hivi kanisa ndo limekuwa dampo ya mavazi na mitindo iliyokataliwa hadi na serekali huku ukijitia moyo kuwa MUNGU anaangalia roho?
Ndungu yangu badilika vaa mavazi ya heshima na yanayokubalika kwa MUNGU na kwajamii husika.....


πŸ‘ ndungu yangu acha kuvaa mavazi ambayo yanakufanya uwe kero kwa MUNGU, wazazi na jamii... Vaa mavazi ya adabu na heshima...


πŸ‘‹⛪ ndungu yangu MUNGU anaangalia mwili na roho... Kumbuka mwili ni hekalu lake, 1 Wakorinto:6.19 Au hamjui ya kuwa Smwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
KUBALI KURUDIWA NA BWANA...
Mithali:3.12
Kwa kuwa Bwana ampendaye humrudi, Kama vile baba mwanawe ampendezaye.

FAHAMU HILI:
kuna mitindo mingi sana duniani kila mtindo unabuniwa kwa malengo na makusudi maalum.
kuna mengine imebuniwa kwa lengo la kuwavuti wanaume kimapenzi (kuamsha tamaa za mwili), hasa mavazi ya kike. wanamitindo duniani wanazidi kubuni mavazi Ya wanawake yenye mvuto wa kimapenzi kwa bei ndogo Zaidi, ili hata mwenye uwezo mdogo Anunue. mavazi hayo mengi ni yale yasiositiri miili yao vizuri, naam ziko zingine ni ndefu paka chini ila inayochora miili yao kama ilivyo na kuchora mistari ya nguo za ndan nk.
NAONGEA NA WEWE DADA:
nini kinakusukuma kuvaa mavazi unayovaa?
je kanisani ni sehemu sahihi ya kuamsha Tamaa za mwili?
1timotheo 2:9-10 ;vivyo Hivyo WANAWAKE Na Wajipambe Kwa Mavazi YA KUJISITIRI Pamoja na ADABU nzuri,....; NB.
Pigia Mstari KUJISITIRI NA ADABU NZURI,


Kumbe unaweza kuvaa mavazi ya kujisitiri yasiwe na adabu nzuri.
JE WAYAFAHAMU MAVAZI YA KUJISITIRI?
MAVAZI YAWEZA YAKAWA YAKUJISITIRI ILA YASIWE NA ADABU NZURI.
Biblia Na Jamii Inayatambua Mavazi Hayo Na Kuyakubali. Je Ujawahi Sikia Watu Hufungwa Kanga Kwenye Baadhi Ya Makanisa Wanapoingia Na Mavazi Yasiositiri Miili Yao Na Ya Siyo Na Adabu?


WAZAZI, JAMII NA VIONGOZI WA DINI WAMEYAKEMEA VIKALI MAVAZI YASIYO NA ADABU,
@Utaendelea kujifariji hadi lini? kuwa MUNGU ANAANGALIA ROHO NA ASHUGHULIKI NA MWILI,?
Ndungu zangu tubadilike, tufuate kile ambacho Mungu amesema na si kufuata hisia na mihemko yetu.

HUJACHELEWA MFANYE KRISTO YESU KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO SASA.

Kwa Yesu kuna raha, hakika tunafurahia wema wake hasa msamaha wa dhambi na uhuru toka kwenye vifungo vya dhambi na kila aina ya uonevu wa shetani. (karibu kwake naye atakuweka huru)


AKILI ZENYE AKILI HUTAFAKARI HAYO
JIULIZE KWA UPOLE hivi mimi ni kilaza wa aina gani hadi nisitambu mavazi ya kikahaba, kulalia, kuogelea n.k? #iulize jamii,

 

Kama Bado ujamwamini na kumkiri YESU kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha fanya uamuzi sasa.

 

 

 


Prepared

By:  Emanuel   ISRAEL  kangala

MOB NO: +255742859313

EMAIL: emanuelkangala@gmail.com

blog:  emaisra.blogspot.com

 


 




UNAWEZA SHARE NA WENGINE: WEWE NI WA BARAKA SANA:


No comments:

Post a Comment