UTANGULIZI
Tunafahamu vyema kuwa panga hutumika kukatia kuni na kufanyia kazi zingine za nyumbani. Alietengeneza Panga alikusudia litumike kwa namna hiyo. Lakini panga linaweza kutumika kuondoa uhai wa mtu ambae ni kinyume kabisa na kusudi la mtengenezaji.
Kumbe Kitu kinaweza kutengezwa kwa kukusudia kusaidia lakini anaekitumia akakitumia kwa kuumiza wengine au kujiumiza mwenyewe. Gari ni zuri na alietengeneza alilitengeneza kwa kusudi zuri lakini likitumiwa bila kufuata utaratibu linaweza kusababisha kifo au maumivu makubwa kwa mtumiaji.
Ndivyo ilivyo ndugu yangu Mungu aliyagawanya majira na nyakati na kutupa uwezo wa kuikumbuka jana au majira na nyakati zilizopita, naam hata uwezo wa kuhifadhi hayo matukio kwa vizazi vingine ili tuitumie leo yetu vyema kwa kujifunza kutoka kwa waliotutangulia au matukio ya Jana. Maumivu au mafanikio yetu ya Jana yanapaswa kuwa sababu ya kufanikiwa kwetu leo na sio sababu ya kufeli kwetu.
Kwa kutokujua namna ya kutumia matukio na kumbukumbu zilizopita ndio sababu ya maumivu mengi tunayoyaona na Wengine tumeshindwa kupiga hatua kwaajili ya Jana Yetu. Badala ya Jana kuwa sababu ya kufanikiwa leo imekuwa sababu ya kushindwa kwetu.
"Matumizi mazuri ya Jana (kumbukumbu na matukio yaliyopita) yako yatakupeleka kwenye utoshelevu na matumizi mabaya ya Jana (kumbukumbu) yako yatakupeleka kwenye uhitaji, kufeli na kukata tamaa. Amuua kuitumia vyema Jana yako Leo kwa manufaa ya Kesho yako."
Tunayoyakumbuka leo ni mambo ya Jana, tulioyafanya, tuliyofanyiwa, tuliyoyasikia na tuliyoyasema, tuliyoyaona na tulioyaonyesha, tuliyotendewa na tuliyoyatenda. Kumbukumbu ya mambo haya yanaweza kukufanya ufanye maamuzi yatakayoijenga au kuibomoa kesho yako.
Unakumbukumbu gani? Unachokikumbuka unakitumiaje kwaajili ya kuijenga kesho yako?
Kwenye maandiko matakatifu kuna mahali Mungu anasema "Usiyakumbuke mambo ya zamani......" Hapa alikuwa anamaanisha nini? Je nauweza nikasahau maumivu niliyopitia jana?
Mafanikio yangu ya JAna yanaweza kuwa kikwazo kwa mafanikio yangu ya kesho?
Kufeli kwangu au kushindwa kwangu Jana inaweza kuwa sababu ya kushindwa kwangu leo? Historia na kumbukumbu ya Jana inweza ikaathiri vipi Leo yangu na Kesho yangu? kivipi? (Usikose sehemu ya pili ambapo tutayaangalia maswali haya muhimu ili kujua namna ya kutumia Jana yangu ili kujenga kesho yenye utukufu.)
Tuangalie sehemu hii ya kwanza ya namna ya kuitumia Jana yako kama Mungu alivyoikusudia ilikuijenga kesho yako.
SEHEMU YA KWANZA (utangulizi)
JANA itufundishe namna ya kuishi
leo, ili kesho yetu iwe yenye utukufu.
Jana au
matukio yaliyopita kwenye maisha yetu, yawe mazuri au mabaya, yanapaswa yatufundishe
namna ya kuishi leo ili kuifikilia kesho yenye utukufu. Hivyo kila unapoangalia
nyuma, utakayoyaona yakufundishe namna ya kuishi leo, yakutie moyo kuendelea
mbele Zaidi, ya kupe ujasiri wa kupambana Zaidi, Mengine yakufanye uongeze
juhudi kwa kuichukia hali ile ya mwanzo na kutaka kuwa bora Zaidi ya Jana yako.
Kuna mambo tunapaswa kuyakumbuka
ili yatupe nguvu ya kukabili changamoto tunayokumbana nayo sasa.
Usiwaogope, kumbuka sana Bwana Mungu wako,
alivyomfanya Farao na Misri yote. (Kumbukumbu 7:18)
Embu kumbuka namna MUNGU
alivyokusaidia na kukupitisha kwenye changamoto ulizopitia, Namna alivyopigana
na adui zako na kulidhibitisha Neno lake Juu yako. Hata sasa usiogope
changamoto unayoipitia bila kujali ukubwa wake, KUMBUKA yale MUNGU
aliyokutendea tangu ukiwa mtoto hata sasa, alivyokutetea shuleni, chuoni,
kazini na kwenye maisha yako kwa ujumla. Hata sasa atakutetea tena. Usiogope
Endelea mbele, usiache hiyo Biashara kwasababu ya hiyo changamoto, usiache
huduma kwasababu ya changamoto hiyo. Endelea mbele PANGA VITA UPYA Mungu yuko
upande wako.
(Usitishwe
na ukubwa wa Goliatia kumbuka Mungu alivyowatia DUBU na simba mikononi mwako,
Hata huyu mfilisti atakuwa kama mmoja wao.)
Unachangamoto
kwenye Huduma yako au Biashara?
Kumbuka
aliekuruhusu uanze hawezi kukuacha uishie njiani, Songa mbele.
Je kila siku unaona kufeli kwenye
biashara yako? Au Taasisi unayoiongoza?
Kumbuka
wanawa Israeli walipigwa na ndugu zao Zaidi ya mara tatu, Baada ya MUNGU
kuwaruhusu kupigana nao. Waamuzi 20:1-48, 21..(stori nzima iko hapa)
Usihofu,
usikate tamaa bali badili mbinu ya namna ya kufanya biashara unayoifanya, namna
unavyotatua matatizo yanayoibuka katika taasisi, jitahidi kuwa muwazi kwa
unaowaongoza. Tumia muda wa kutosha kufikiria juu ya taasisi na namna ya
kuboresha kwa maslahi mapana ya Taasisi.
Jitahidi
sana makosa uliyoyafanya jana yasijirudie leo, nayale mazuri ya jana uyaboreshe
leo.
(Basi kumbuka ni wapi ulikoanguka, ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza,
lakini usipofanya hivyo, naja kwako, name nitakiondoa kinara chako katika
mahali pake, usipotubu. ufunuo2:5).
Badilika
fanya tofauti na ulivyofanya jana.
Unataka kuoa au
kuolewa na unahisi muda umeenda sana na bado huelewi?
Kumbuka
Kisima kipo mbele yako upo karibu sana na kijito cha Maji kama Hagai, Macho
yako yakafumbuliwe, Ukaone vyema.
Je Familia
imekutenga na kukuchukia bila Sababu?
Mkumbuke
Yusufu pamoja na kutengwa na familia yake haikuwa sababu ya yeye kuizika ndoto
yake. Kumbuka MUNGU anakupenda usijichukie hata wote wakikuchukia, Kaza mwendo
kuikabili hali yako ili jina la Bwana litukuzwe kama lilivyotukuzwa kupitia
YUSUFU.
JE kazini wamekusingizia?
Umefukuzwa kazi Bila sababu?
Kumbuka Yusufu alifukuzwa kwenye nyumba ya Potifa na kutiwa gerezani, na Hiyo ndiyo iliyokuwa hatua yakuelekea IKULU na kuiongoza nchi nzima ya MISRI. Inawezekana kufukuzwa kwako kwa kuonewa ndio sababu ambayo MUNGU anaitumia ili kukuinua Zaidi.
#inuka tena Acha kulia
#Fanya kiume.
Tujifunze kwenye
historia yetu naya wliotutangulia na sio kudumu kwenye maumivu ya Jana.
#Wewe ni wa thamani
sana hii ndio sababu, bila kujali makosa na dhambi ulizokuwanazo YESU alikuja
na kufa msalabani kwaajili yako.
TIPS:
1. 1. Hauruusiwi
kukata tamaa kwenye kuuendea ukuu wako, Bila kujali ukubwa wa changamoto
unayokutana nayo.
2. 2. Ukifeli kwenye kitu au biashara unayofanya haimaanishi kwamba
wewe ni kilaza Bali inamaana badili njia ya kufanya.
3.
3. Kumbuka
hauruhusiwi kufanya kila kitu kwasababu wengine wanafanya, Bali kuna wakati utapaswa
kujinyima ili kuifikilia ile thawabu iliyo mbele yako. 1cor 9:25
4.
4. Kuna
kumbukumbu zingine zinaumiza ila unapaswa kuzikumbuka ili zikupe nguvu ya
kuendelea mbele, nguvu ya kuongeza mwendo Zaidi. Na ujasiri wa kutokukata tamaa
wala kutamani maisha ya jana. Hasa kukumbuka namna ulivyotoka au namna ya
kutoka na namna unavyotakiwa kuishi iliusirudi kwenye maumivu ya jana.
Kumbukumbu 16:12 “..Nawe kumbuka kwamba
ulikuwa mtumwa huko misri, tena zishike amri hizi kwa kuzifanya” Kumbukumbu
24:18, 22
5.
5. Kuna wakati unapaswa kukumbuka namna ulivyoanza, ulivyopokea, na
jinsi ulivyosikia ilikujua wapi ulikosea au unapopaswa kuongeza juhudi au
kuboresha Zaidi ili kuijenga kesho yenye utukufu. ( “Basi kumbuka jinsi ulivyopokea na jinsi
ulivyosikia, yashike hayo na kutubu …..” Ufunuo3:3
“Basi kumbuka ni wapi ulikoanguka ukatubu ukafanye matendo ya
kwanza….” Ufunuo 2:5
INAENDELEA,
USIKOSE
SEHEMU YA PILI.
IMEANDALIWA
NA
EMANUEL
ISRAEL KANGALA
0742
859 313
Website:
EMAGK SITE.
Url:
Emaisra.blogspot.com
13MAY 2022.
No comments:
Post a Comment