HEKIMA ZA MZEE 2060.
Mzigo huu utaubeba mwenyeweee.... Sauti ya mzee ilisikika
Panapohitajika maamuzi ni wazi kabisa kuna cha kubeba na kuacha na hapa ndio mtihani huanzia.
Mzee alinisogelea akanishika bega akaniambia...
mwanangu;
Madhara au matokeo ya chochote unachokifanya utayabeba wewe mwenyewe, hata waliokushawishi hawatakusaidia...
Kumbuka
[ haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake.)Ezekieli 18:20, Wala hautakuwa juu ya washauria wake au walimu wake, Nisikilize Emanuel
(hapa mzee alikazia na alitaka nifahamu maamuzi nitakayofanya ninapaswa kuangalia kwa makini matokeo badala ya watu watanionaje? )
Mzee aliniangalia kisha akasema Mwanangu unaruhusiwa kuomba ushauri, lakini kupewa ushauri bila kuwa na hekima ya kuchuja na kupambanua vyema ni sawa na kupelekwa kwenye mzinga wa nyuki ukitamani kula asali yake lakini usijue namna bora ya kurina asali ile. si unajua ukikosea kuirina unaweza ukajikuta utatoka na maumivu au kifo kabisa bila hata kuionja asali yenyewe.
Ndo maana wazee walisema akili za kuambiwa changanya na zako, ila kumbuka sulemani alisema na kuonya usizitegemee akili zako mwenyewe. mithali 3:5, 23:4
Kumbuka Ni muhimu Sana kuwa na washauri, maana ili ufike mbali UNAHITAJIKA washauri si washauri tu Bali washauri wenye akili.
Mithali 15:22
[22]Pasipo mashauri makusudi hubatilika;
Bali kwa wingi wa washauri huthibithika.
Mwanangu kumbuka mshahara wa dhambi Ni mauti haujawahi kubadilika.
Ni wengi wanaoweza kukushawishi kufanya dhambi, lakini kumbuka wewe ndie utakaebeba matokeo ya hicho utakachokifanya.
[Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, Wewe usikubali.)Mithali 1:10
Kwa ushawishi mkuu wa marafiki ukaacha kusoma shuleni, ukawa kinara wa kudhurura, bangi, mirungi, uzinzi, baada ya kufukuzwa shule maaumivu yake utayabeba mwenyewe.
Maumivu na matokeo ya kufeli hakuna atakaekusaidia kubeba zaidi yako wewe mwenyewe.
Watakubebeleza kufanya uzinzi, lakini ukipata mimba au magonjwa ya zinaa watakuwa mbali na wewe. ( They will not be there for you)
Wala hawana uwezo wa kukusaidia kubeba maumivu ya matokeo utakayopata kwa wakati huo. Hata Kama wakitamani kufanyahivyo.
Watakubebeleza kwa ushawishi mkubwa uonyeshe utomvu wa nidhamu kwa boss wako kwa sababu Fulani, lakini atakaefukuzwa kazi Ni wewe Wala si wao. Nakuambia hata kutoa Mia yao hawatatoa kwako, ila wanaweza kuishia kukuita mjinga, Kuwa makini Emanuel.
Chochote unachokifanya Sasa kinamatokea baadae mazuri au mabaya kulingana na unayofanya.
Kumbuka maamuzi mazuri mazuri na ya busara unayotoa yanatokana na maarifa uliyonayo juu ya Jambo husika.
Kumbuka
kila unapofanya maamuzi zingatia matokeo badala ya kuangalia ushabiki na kuwaridhisha watu, kwani atakae umia au kufurahia matokeo ni wewe mwenyewe.
Mzee alinitazama Sana kwa makini mda huu alitwaa glass ya maji ya baridi iliyokuwa pembeni yake na kupiga pafu mbili Kisha akanishika bega na kusema mwanangu Kati ya maamuzi ya pekee na yamuhimu unayopaswa kufanya Ni kuhusu hatima yako baada ya maisha haya.
Kifo Ni uhakika na sio imani kwa yeyote aliezaliwa na Alie na mwili, haikanushiki lazima kuna siku utakufa. Je unauhakika na maisha yako baada ya kifo.
Unauhakika utakuwa sehemu salama baada ya kifo chako? Uwe na uhakika mwananguuu baada ya starehe zote, kuwa na mke mzuri au mume mzuri, kumiliki magari, private jet na vitu vya kifahari, Kuna siku utakufa.
Umejiandaa aje na maisha baada kifo.
Hapa nilimuangalia mzee na kumjibu kwa ujasiri mkubwa Sana kuwa Mimi Ni mtu wa Dini na nafuata sana kanuni na SHERIA za Dini yangu hivyo nafikirii baada ya kifo bado nitakuwa sehemu salama.
Mzee alinikazia macho akaniambia hapo sio swala la dini Kila mmoja ana dini yake, hata kabla ya hizi zilikuwepo dini zingine.
Nazungumzia swala la uhakika wa maisha yako ndani ya moyo hata ukifa leo. Je ukifa leo unauhakika wa kwenda Mbinguni?
Nisikilize Yuko aliyenipa uhakika na kuniondolea hofu ya kifo ndani yangu toka ujana wangu Hadi Sasa siogopi kifo kwani Nina uhakika na maisha yangu baada ya kifo, maana amenihakikishia ndani ya moyo wangu, sio kwa maneno matupu au ahadi tupu Bali kwa udhibitisho wa kweli na ushuhuda wa kweli ndani ya moyo wangu unaonipa ujasiri wa kusimama na kuwa na uhakika na kesho yangu bila kuogopa kifo.
Nilidakia kwa haraka Mzee naomba uniambie maana kweli binafsi uhakika nilionao Ni was mdomoni na faraja lakini Kila nitamkapo moyo haupo pamoja na Mimi. Nisaidie mzee na Mimi nipate uhakika upionao wewe ili baada ya maisha haya niyafurahie maisha.
Mzee aliniangalia akaniambia maamuzi ni yako Nafikiri umezisikia habari za YESU yeye ndiyo njia na kweli na uzima. Anatuhakikishia yote kwa Roho wake mtakatifu anaekaa ndani yetu kwa Kila amwaminie, hivyo uchaguzi Ni wako mpookee leo akuhakikishie uzima wa milele. Uwe na uhakika na kesho yako.
Fanya uamuzi Sana, maana matokeo ya uamuzi huu was kumkubali au kumkataa utabeba mwenyewe. Na matokeo yake Ni makubwa ajabu...
Mzee aliinua glass yake ya maji na kuingia zake chumbani.
IMEANDALIWA NA
EMANUEL ISRAEL KANGALA
No comments:
Post a Comment