NAMNA YA KUYAFIKIA MALENGO YAKO - EMAGK SITE

Latest

This website was designed to help college student especially those who takes engineering course for review, past paper and other learning material. And teacher for review.

Sunday, June 1, 2025

NAMNA YA KUYAFIKIA MALENGO YAKO

 

Malengo yanakuonyesha hatma mwisho wa safari yako, ila kitakachoamua umbali na wapi utafika inategemea sana hatua zako nayale unayoyafanya kila iitwapo leo. Kwani unachokifanya leo ndio kinachotoa muelekeo na kuamua hatma yako.

Hatma yako haiamuliwi na malengo uliyonayo pekee bali hudhibitishwa nayale unayoyafanya kila iitwapo leo.

Mungu anaangalia sana leo kuliko jana yako.

Kabla hujasema ni mapenzi ya MUNGU unapaswa kuangalia kwanza hatua zako, ili isije kuwa yale uyafanyayo kila siku ndio yaliyokufikisha hapo tofauti na maono na ndoto ulizonazo.

Kilichomfanya Sauli aondoke madarakani sio Mapenzi au Mpango wa MUNGU bali ni yale aliyoyafanya kila siku.

Kosa la kwanza ni kosa lakini kurudia kosa ni mchakato wa kutengeneza tabia. Na ikumbukwe Ni rahisi sana kurekebisha kosa na sio tabia.

Sauli alipokosea akutubu na kuacha kosa, Bali aliendelea kulifanya lile kosa lilofanya akose vigezo vya kuendelea kuwa mfalme wa Israel.

Daudi Baada ya kukosea alijuta akatubu kwa machozi na hakurudia tena kosa hilo, hili lilimfanya adumu kwenye ufalme wake, Na MUNGU afurahie sana.

Tatizo sio kosa ulilolifanya tatizo limegeuka kuwa tabia na hauko tayari kuiacha.

Toba ni kubadili mwelekeo wako na hatua zako upigazo, hivyo hatutegemei baada ya toba uendelee kwenye njia ileile ya mwanzo. 

Ukirudia njia ileile tegemea kuvuna sawasawa na matendo yako, na utafika sawasawa na uelekeo wako.


Zaburi 1:1-

Mwanzo mtunga zaburi anaelezea hatua za huyu mtu, mambo anayoyaepuka na mambo anayoyafanya na mwisho anaelezea hatma yake.


Hivyo hatma ya mtu haitegemea shauku yake, maono yake na ndoto zake, ingawaje hayo yote ni yamuhimu katika kuziongoza hatua zake.

Hatma yako inategemea sana hatua zako na uamuzi wako wa kutokutenda tofauti na maono na ndoto zako.

Adui akitaka kuipiga kesho yako, atapiga hatua zako. Maana yale unayoyafanya leo ndio yanayoamua uelekeo na hatma yako ya kesho.

Atahakikisha anapiga Tabia yako, maana ni moja ya hatua zako zakukufikisha uendako au kukupoteza.

Mwanangu niamini mimi hakuna asiyekuwa na maono, ila yupo anayeyapinga maono yake kwa yale ayafanyayo. Eidha kwa kujua au kutokujua.

Ila kumbuka unapompinga shetani, kumkemea na kumfukuza usisahau kuangalia sana uliposimama, usije ukawa unamkataa kwa maneno lakini matendo na mtazamo  wako unamkaribisha kwa deremo na vifijo.

Kurelax na kuendelea kufanya kosa ulilolifanya ni njia mojawapo ya kuzika kesho na maono yako.

Mwisho wa vita ni mmojawapo wa wapiganaji kujisalimisha, ILI vita iishe ni lazima mmoja ajisalimishe au ashinde kwa nguvu. Ukijisalimisha tu kwenye dhambi inayokutesa kwa kuona hakuna namna ya kutoka basi Jua vita yako na dhambi imeisha, umeshashindwa, na dhambi imeshinda upande wako. Hivyo tegemeao malipo yake.

PIGANA VITA, ACHA UZEMBE WA KUKUBALI KUSHINDWA KIRAHISI WAKATI YUPO ALIE MKUU ZAIDI YAKO APIGANAYE UPANDE WAKO.

Itaendelea



EMANUEL ISRAEL KANGALA 

No comments:

Post a Comment